Chromebook ni kompyuta mpakato (Laptop) zenye sifa nzuri na nyingi zinasifika na kuwa na umbo dogo na vile vile hata kuwa na bei ndogo –japo zipo za bei ya juu—ukilinganisha na zingine.
Kompyuta hizi –za Chrome – kwa kawadia huwa zinatumia program endeshi inayojulikana kama Chrome OS ambayo mara kwa mara imekua ikifanyiwa maboresho na kuengezewa baadhi ya vipengele.
Kwa kompyuta ambazo zinatumia Windows au hata MacOs huwa zinakuja na folder maalum ambalo huwa linahifadhi mambo yote ambayo yamefutwa katika kompyuta hiyo.
Google hivi karibuni tuu wameachia toleo jipya la kivinjari chake cha Chrome na muda tuu ulivyopita wakaamua kuachia na sasisho jipya la Chrome Os katika vifaa vya Chromebook.
Toleo hilo jipya lina maboresho katika maeneo ya keyboard, kamera uwezo wa ku’scan, uwezo wa kukamata WiFi kwa haraka na mengine mengi bila kusahau Folder la taka –vitu ambayo umevifuta.
Tofauti ya Folder katika programu endeshi ya Chrome Os na zingine kama vile Windows Os Na MacOs ni kwamba hapa mafaili yataweza kufutika yenyewe ndani ya siku 30.
Hii haina tofauti kabisa na huduma ya Trash katika mtandao wa Gmail maana barua pepe ambazo umazifuta huwa zinaenda kukakaa katika sehemu ya Trash na baada ya mwezi huwa zinajifuta.
Kingine kizuri ni kwamba kama ukighairi jambo hili unaweza ukaingia na kurudisha mafaili yako katika Folder lake ambapo ulilifutia –-Japo hii iko kwa programu endeshi zote.
Folder la uchafu (Trash Folder) limekua likifanyiwa kazi na majaribio tangia mwaka 2020 mwezi oktoba na kwa kupitia sasisho jipya la Chrome Os watumiaji wataweza kunufaika na hili.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je ushawahi kutumia Chrome Os? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment je uzoefu wako ukoje na vile vile niambie kama utaweza pata sasisho hili na kuendelea kufurahia huduma hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.