Programu tumishi-Clubhouse ni maarufu kwa watu wengi tuu duniani na sasa imeonekana kuwa inafaa ipatikane kwa watumiaji wa Android pia.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja programu tumishi-Clubhouse imekuwa ikipatikana kwenye iOS pekee na hivyo kuifanya kuwa na watumiaji kutoka upande mmoja tu. Hilo limebadilika kwani sasa yafika kwenye Android pia. Ndio, Clubhouse ni programu tumishi lakini je, inahusika na nini hasa?
Huu ni mtandao wa kijamii ambao unaruhusu watumiaji kuweza kutengeneza chumba cha mazungumzo ambacho watu wanaweza kuingia kwa kualikwa na kusikiliza kipindi kwa njia ya sauti ambacho mtu anakuwa amekiandaa.
Clubhouse yafika kwenye Android: Vipindi vinavyorushwa ndani ya programu tumisihi husika ni mubashara na hawezi kurekodiwa kwa ajili ya kusikilizwa baadae.
Ile ya kwenye iOS ina vitu vilevile ambavyo vipo kwenye Android kwa maana ya kwamba inabidi mtu kualikwa ili aweze kuikingia ndani ya chumba kuweza kusikiliza kile ambacho kipo hewani (mubashara) kwa muda huo. BOFYA HAPA kuweza kufahamu mengi zaidi kuhusu programu tumishi husika.
Katika siku za karibuni programu husika imekuwa na watumiaji wachache na hatua hii ya kupeleka mtandao wa kijamii kwenye Android hakika utaongeza watu wengi.
Daima tunahakikisha kuwa masomaji wetu wanahabarika kila siku. Je, una swali au maoni? Basi usisite kutuandikia nasi tutakujibu.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
No Comment! Be the first one.