Miaka 30 iliyopita siku ya jumapili tarehe 15 machi 1985 anuani ya kwanza ya .Com ndio iliandikishwa, tukio hili lilibadilisha teknolojia ya intaneti kwa ujumla.
Anuani ya ‘domain’ ya .Com haikukua kwa haraka miaka hiyo na ukiangalia hata mfumo wa ‘www.’ ulikua bado haujagunduliwa (hakuwepo kipindi hicho). Mpaka mwaka 1987 kulikua na anuani 100 tuu za .Com. Lakini kwa hivi sasa kila sekunde kuna anuani mpya ya .Com inayoanzishwa. Kwa mahesabu ya haraka kwa siku zinatengenezwa anuani za mitandao 80,000!
Mwaka 1987 ndipo makampuni makubwa yalipoanza kufungua macho na kujua kwamba teknolojia ya intaneti inaweza kutoa mchango mkubwa katika biashara zao na mchango huo utawasaidia kupata faida kwa kiasi kikubwa. Makampuni kama Apple na Sisco kwa kufuatana walijiunga kwa kutumia ‘domain’ ya Apple.com na Sisco.com mwaka 1987.
Mnamo mwaka 1991 The World Wide Web (www) ilizinduliwa na kuanza kutumika rasmi. Teknolojia ya Www iliwezesha na inawezesha watu hadi leo kuweza kutumia mitandao ya dot com na mingine mingi tu kwa sasa.
Mwaka 1994 mtandao nguli wa Amazon ulitumia ‘Domain’ ya .Com na kuanza kutumika rasmi hiyo ni mwaka mmoja baada ya mitandao kama Yahoo na AOL ikajiunga. Yahoo mara ya kwanza ilianzishwa na kupewa jina la “Jerry and Dave’s Guide to the World Wide Web”na baadae ikabadilishwa na kuwa Yahoo mwaka huo huo.
Mara tuu baada ya mwaka 1996 Hotmail.com ilianzishwa na pia hata Expedia.com ambayo ilibadilisha kwa kiasi kikubwa jinsi ya kukata tiketi za safari ki mtandao.
Mwaka 1997 Netflix.com ilianzishwa na baada ya mwaka Google.com ikawa hewani na kubadilisha jinsi ya kupata taarifa mbali mbali katika mtandao (Intaneti).
Mitandao mingine mikubwa iligunduliwa mfano Skype.com ilianzishwa mwaka 2003 ambayo inahusisha kupiga na kupokea simu kimtandao (online). Mwaka 2004 Thefacebook.com ilianzishwa ambayo baadae ilibadilishwa jina na kuwa facebook.com. Youtube,Com ilienda hewani mwaka 2005 na baada ya mwaka tuu mtandao wa Twitter.com ukawa hewani tuu.
Heri ya kuzaliwa .com 🙂
No Comment! Be the first one.