Siku ya jana, Ijumaa ya tarehe 19 Julai, 2024 watumia wengi wa Microsoft duniani kote walikumbwa na matatizo makubwa ya programu endeshaji baada ya hitilafu katika sasisho la programu ya usalama ya CrowdStrike. Programu hiyo hutumika kuwalinda watumiaji wa Microsoft dhidi ya virusi.
Hitilafu hiyo ilisababisha kuzorota kwa programu na huduma mbalimbali za Microsoft 365, ikiwa ni pamoja na Outlook, Teams, na PowerBI. Hii ilisababisha misururu mirefu kwa mashirika na biashara nyingi zinazotegemea programu hizi kufanya kazi zao.
Sekta mbalimbali muhimu kama vile za kibenki, televisheni, afya na usafiri hasa wa anga na zingine zote zinazotegemea mifumo ya kikompyuta katika ufanyaji kazi ziliathirika sana. Ukitoa changamoto zilizotokea nchini Tanzania, nchini India pekee, ndege zaidi ya 1000 zilisitishwa kutokana na hitilafu hiyo.
CrowdStrike imethibitisha hitilafu hiyo na inafanya kazi kuitatua. Microsoft pia imetoa taarifa ikisema wanachukua hatua kurekebisha tatizo na wameridhishwa na juhudi za CrowdStrike.
CrowdStrike ni nini?
CrowdStrike ni programu ya utoaji huduma ya ulinzi kwa kompyuta na mifumo ya kikompyuta inayotumiwa na biashara mbalimbali katika kulinda mifumo yao dhidi ya udukuzi.
Tatizo lilianzishwa na nini?
CrowdStrike walituma masasisho ya programu yao ambayo yalileta hitilafu ya kutoelewana na mifumo mikubwa ya uendeshaji ya programu endeshi ya Windows. Tatizo lilikuwa kubwa kiasi cha kompyuta kujilinda kwa kujizima na kukataa kuwasha programu endeshi – kompyuta zikiwaka ziliishia eneo la kushindwa kumaliza utaratibu wa kuwaka ambalo ni maarufu kwa jina la ‘windows of Death’
No Comment! Be the first one.