Je ushawahi kujiuliza kwa nini diski zinaanza na namba C badala ya A kwenye kompyuta zinazotumia Windows? Leo fahamu.
Kwa watumiaji wa kompyuta wa tokea miaka ya 90 ni rahisi wao kuelewa sababu, au kutojua sababu ila washawahi kutumia kompyuta wakati diski zinatambulika pia kwa namba A.
Historia
- Programu endeshaji ya Windows ilitengenezwa juu ya mfumo endeshaji mwingine wa kwanza kutoka Microsoft uliokuwa unatambulika kwa jina la MS-DOS. Kipindi hicho mfumo wa diski za flopi ndio zilikuwa zinatumika (floppy drives).
Je kwa nini diski zinaanza na namba C badala ya A?: Muonekano wa diski za Flopi - Katika kompyuta hizo kompyuta ilikuwa ina uwezo wa kutumia hadi diski za flopi mbili kwa wakati mmoja na hivyo moja kwa moja ya kwanza ilichukua nafasi ya utambulisho wa A: na ya pili ikachukua nafasi ya utambulisho wa B:.
Baadae diski za mfumo wa ‘harddrives’ zilivyokuja ndio zikachukua nafasi ya C:, na mgawanyo wa diski (partition) wa pili au diski nyingine ndani yake ndio ikachukua nafasi ya D:, sehemu ya cd, yaani CD-ROM ndio ikapewa nafasi ya E:
Hiyo ndio historia fupi na sababu kuu kwa nini diski kwenye kompyuta yako kwa sasa zinaanza na kubeba namba C:, ila kumbuka teknolojia ya utambuzi wa diski za flopi bado upo kwenye Windows. Mfano ukiwa na kimashine cha kutumia flopi na ukakipachika kwenye kompyuta yako basi flopi itatambulika kwenye Windows na itachukua namba A:
