Kampuni la magari maarufu, Ford limeweka wazi mipango yake ya kufungua kiwanda kikubwa cha kuzalisha magari madogo huko Mexico. Ford tayari imetenga kiasi cha dola bilioni 1.6 za kimarekani kwa ajili ya kuliwezesha hili
Kiwanda hicho kama mikakati yake ikienda vizuri kitaanza kuzalisha magari mwaka 2018. Japokuwa kampuni lina mikakati mizuri lakini bado mkakati wao huo unapata wakati mgumu baada ya kupata changamoto kubwa baada ya watu wengi ikiwemo mgombea urahisi kupitia chama cha ‘ republican’, Donald Trump
Donald Trump anaona mpango huo mzima kama upuuzi tuu na amesema kama akifanikiwa na akashinda kama Rais basi kamwe jambo hilo hataliruhusu.
Kampuni la Ford kwao wanaona ni jambo jema kufungua kiwanda hicho kwani mpaka kufikia mwaka 2020 tayari kampuni litakuwa limeshatengeneza ajira 2,800 – ukiniuliza mimi hii ni namba kubwa sana ya ajira kwa kiwanda kimoja — mpango huu unaaminika kuwa ambao utafanya kampuni liweze kutengeneza magari magodo madog (bei ya chini)
Japokuwa kampuni halijaweka wazi kuwa ni aina gani za magari ambayo yatakuwa yanazalishwa katika kiwanda hicho. Raisi wa ‘United Auto Workers’ (UAW), Bwn Dennis Williams amesema kuwa uwamuzi wa kampuni hilo kufungua kiwanda huko mexico sio mzuri kwani kampuni lingeweza kufungua kiwanda US na wakazi wa marekani wakafaidika na nafasi za ajira kutoka katika kampuni hiyo.
“Makampuni yamekuwa yakikimbilia katika nchi ambazo zina nguvu kazi ya chini na yakimaliza kutengenza bidhaa zao yanarudi nyumbani (US) kuja kutafuta soko. Hili linabidi likome” – aliongezea Bw. Williams
Bw. Trump amekuwa akipinga vikali kwa makampuni ambayo yanataka kuwekeza nchini Mexico akiwa anaamini kuwa nchi yao ya nymbani itakosa mapato makubwa
Kama akipata uraisi ameahidi atahakikisha hakuna biashara itakayofanyika kwani anaweza akaizuia. Licha ya hayo yote kampuni la Ford bado limesimama katika misingi yake ile ile ya kufungua kiwanda hicho nchini Mexico.
Kampuni imeongezea kuwa sio kwamba nchi hiyo (Mexico) ina nguvu kazi ya hali ya chini bali hata upatikanaji wa malighafi zingine ni rahisi sana na kikubwa ni kwamba wana sapoti kubwa kutoka katika serikali yao.
Pia kampuni ya Ford imesema isingependa kuonekana kama inaisaliti US kwani kuanzia mwaka 2011 mpaka 2015 ilikuwa tayari imeshawekeza Dola bilioni 10 za kimarekani ambazo zilitengeneza kazi 25,000 kama kazi ambazo ziliongezeka.