Raisi wa zamani wa marekani alizuliwa/alisimamishwa kuingia na kutumia mitandao yake ya kijamii Facebook na Instagram mpaka sasa inafikia miaka miwili.
Trump alisimamishwa kutumia mitandao hiyo ya kijamii inayomilikiwa na Meta baada ya raisi huyo wa zamani kukiuka baadhi ya vipengele na ilianzia facebook na baadae ikaenda mpaka instagram.
Kwa sasa Meta wenyewe wametoa taarifa kwamba kufungiwa huko kumefikia mwisho na wana mpango wa kumrudisha katika mitandao hiyo ya kijamii.
Kingine ni kwamba bwana Trump alikua kafungiwa katika mitandao mingine ya kijamii kwa mfano katika mtandao wa Twitter alirudishwa mwaka jana mwezi novemba.
Mitandao ya kijamii huwa ina sera na sharia zake ambazo zinaendesha watu husika katika mtandao wa kijamii na mtumiaji akikiuka vipengele hivyo huwa anachukuliwa hatu na moja wapo ni kuzuiliwa kutumia mtandao huo kwa muda au zaidi.

Trump atarudishwa katika mitandao hiyo ndani ya wiki kadhaa zijazo, hii ni wenyewe Meta ambao wameweka wazi kabisa lakini kama atakiuka tena baadhi ya mambo basi ataweza kufungiwa tena.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Wewe unaonaje je kurudishwa kwa Trump ni sawa?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.