Kama kuna sekta ambayo makampuni mbalimbali wanaiendeleza na kuzidi kukua kwa kasi huwezi kuacha kuongelea ndege zisizokuwa na rubani kwa matumizi yake kushamiri nchi nyingi duniani na kuwa kitega uchumi/chanzo cha mapato kwa watu.
Ndege zinazoendeshwa bila rubani zipo za ukubwa tofauti tofauti; kuanzia ndogo, ukubwa wa wastani na kubwa kabisa zenye uwezo wa kubeba abiria wawili huku malengo yakiwa ni kutengeneza ndege zisizokuwa na rubani zenye uwezo wa kubeba abiria wengi na kufanya safari ndefu.
Ndege hiyo ambayo ni hatua kubwa kwenye masuala ya teknolojia kwa ndege zinazoendeshwa bila rubani halikadhalika zile zinazotumika kupeleka mzigo kwa mteja. Ndege hii mpaka sasa bado haijapewa jina rasmi ila inafahamika kama unmanned electric vertical-takeoff-and-landing (eVTOL).
Drone inayofahamika kama eVTOL ilifaulu majaribio ya mwanzo. Ni moja kati ya ndege kubwa ambazo zitatumika kupeleka mzigo kutoka sehmu moja hadi nyingine.
Iliwachukua wahandisi kipindi cha takribani miezi mitatu kufanikisha ujenzi wa ndege hiyo ambapo kwa muujibu wa kampuni iliyohusika kuitengeneza imekiri kuwa hatua waliyoifikia ni kubwa na ya kujivunia, daima watakumbuka ujenzi wa eVTOL.
Sifa za ndani za ndege kubwa ya kubeba mizigo (CAV).
Drone hii kwa jina lingine inafahamika kama Cargo Air Vehicle (CAV) kwa tafsiri isiyo rasmi ni ndege ya mizigo. Ina mota 8; inafanya ndege hiyo kupaa katika hali ya unyoofu kutoka chini kwenda juu, urefu ni mita 4.57, upana ni mita 5.49, urefu wa kutoka chini kwenda juu ni mita 1.22.
CAV ina uzito wake ni kilo 339 na inauwezo wa kubeba mzigo wa paundi 500|Kg 226.
CAV huwenda zikatumiwa na Uber kutokana na kuwepo ushirika kati ya makampuni hayo mawili hiyo kuifanya Uber kutanua wigo wa biashara yake kwa kuwa na uwezo wa kufanya huduma ya usafirishaji kwa njia ya anga.
Vyanzo: The verge, Aurora
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|