Huduma ya uhifadhi wa mtandaoni ya Dropbox imefikisha watumiaji milioni mia tano ama nusu bilioni. Huduma hii iliyoanzishwa rasmi miaka nane iliyopita inatumiwa kuhifadhi data kama mafaili miziki na picha katika mtandao badala ya kuhifadhi katika kifaa.
Swala la uhifadhi wa mtandaoni ama Cloud storage limezidi kushika kasi na kupata umaarufu baina ya watumiaji wa vifaa vya ki-elektroniki. Hapo kipindi cha nyuma watu walikua wanalipa gharama kubwa kwa ajiri ya kupata vifaa ambavyo vina ujazo (storage/memory) mkubwa zaidi ili kuhifadhi vitu vingi kama picha na nyimbo katika simu lakini kwa sasa jambo hilo linazidi kupotea maana sasa watu wanakimbilia uhifadhi wa mtandaoni.
Zaidi ya sifa ambazo nimezitaja hapo juu pia ukiwa unatumia Dropbox unapata uwezo wa kuzishusha data zako katika kifaaa chochote kile unachotumia ili mradi tu huduma hii ipo katika simu hiyo. Pindi unapopoteza simu kwa mfano basi hautakuwa na wasiwasi maana taarifa zako za muhimu utazipata katika kifaa chako kipya utakacho nunua au kupitia mtandao wao moja kwa moja.
Faili unalolipakia katika akaunti yako katika simu unaweza kulipakuwa katika kompyuta yako ama pia unaweza kulipakua katika kifaa kingine chochote ambacho kina Dropbox.
Japokuwa Dropbox wamefikia mafanikio haya ya kupata watumiaji karibu nusu milioni bado wanakumbana na changamoto kwamba yapo makampuni mengi yanatoa huduma zinazofanana kabisa na zile ambazo wanazitoa wao.
Hii itapelekea kusha thamani ya soko ya Dropbox kitu ambacho sio kizuri kibiashara. Ni wazi kwamba wamiliki na wadau wa Dropbox wataleta mabadiliko mbalimbali ili kuweza kuhakikisha kwamba thamani yao ya soko inabaki kuwa kubwa.
Kama hauitumii huduma hii ni wakati pengine ukajifunza na kujaribu kuitumia maana inaweza kukuokoa nyakati fulani, mfano badala ya kunua simu yenye diski ujazo mkubwa unaweza kununua simu ambayo ina sifa (specifications) sawa ila yenye diski uhifadhi mndogo kwa bei nafuu zaidi huku ukitegemea kuhifadhi data zako kupitia DropBox.