Katika kupambana na matumizi ya sigara za asilia nchini Uingereza na duniani kote, serikali ya nchi hiyo imepitisha matumizi ya sigara zinazotumia umeme. Sigara za umeme maarufu kama e-cigarette, hutumia betri zinazoupa nguvu mvuke ambao humpa mvutaji hisia ya sigara ya kawaida lakini bila kutumia tumbaku.
Badala ya kuvuta moshi wa kawaida wa sigara, mtumiaji huvuta mvuke unaotoka kwenye kimiminika muhimu kijulikanacho kama kimiminika umeme chenye mchanganyiko wa vitu tofauti kama maji, nikotini, glicerini na ladha mbalimbali zinazomvutia mvutaji kwa chaguo lake.
Shirika la Afya la Uingereza limethibitisha sigara za umeme ni salama Zaidi ikilinganishwa na sigara za kawaida kwani zina madhara pungufu ya asilimia 95 kuliko sigara za kawaida. Sigara hizi zinaweza kutumika dhidi ya kampeni ya matumizi ya tobako ambayo ni hatari zaidi kwa matumizi ya binadamu.
Japo sigara hizi zinaweza kuwasaidia watu wazima kuacha sigara za kawaida kabisa, lakini bado kuna haja ya kuhamasisha na kuwaepusha watoto dhidi ya matumizi ya bidhaa hizi kwani hatari huweza kuwa kubwa zaidi.
Nchini Tanzania, sigara za umeme zimeshaingia kwa kasi na kutumika kama mtindo kwa vijana wengi hasa katika kumbi za starehe na hata majumbani. Lakini swali la Msingi kutoka teknokona ni endapo sigara hizi zimeleta ukombozi kwa wavutaji wa sigara au ni majanga mapya kwa vizazi vilivyopo?
Mambo matano muhimu kuyajua kuhusu sigara za umeme ni kwamba;
1. Japo hazitumii tumbaku, Sigara za umeme bado zina nikotini na kemikali nyingine za sumu zinazoweza kumlewesha mlewaji.
2. Sigara za umeme haziwashwi kwa kutumia kiberiti, bali kitufe kidogo cha umeme kilicho kwenye sigara hizo
3. Sigara za umeme huweza kutumika Zaidi ya mara moja na hivyo kuwa na gharama ya chini zaidi kulinganisha na sigara za kawaida.
4. Bado sigara hizi zinaweza zikaathiri mapafu, na zimepigwa marufuku katika baadhi ya nchi duniani.
5. Moshi wake huweza kumuathiri ata mtu wa pili ambaye si mvutaji kama ilivyo kwa sigara za kawaida.
Je una maoni gani kuhusu teknolojia hii ya sigara za umeme? Kumbuka tofauti kuu ni ukosefu wa moshi wenye mchanganyiko wa vitu vingi vyenye madhara mengi, lakini kama vile kwenye sigara ya kawaida ‘nikotini” ambacho ndio kitu kilicho kwenye tumbaku kinapatikana kama kawaida.
Chanzo: The Guardian, The Independent and Google Images.
sasa si soko la tumbaku litapotea kabisa