Teknolojia ya spika za masikioni ambazo hazitumii waya inaonekana kuendelea kupendwa na makampuni mengi wanajitahidi kuja na bidhaa zao katika mtindo huo. Tayari kuna PowerBeats ambazo zimeundwa mahususi kwa ajili ya yeyote anaependa mazozi lakini kuna taarifa Apple wanatoa Beats zisizo na waya mwezi Aprili.
Apple ambao ndio wamiliki wa bidhaa zinazobeba jina la “Beats” wapo mbioni kuzindua spika za masikioni ambazo hazina waya unaoonekana (wireless earbuds) ikiwa ni maboresho kwa bidhaa yao ya sasa, PowerBeats. Hii ni kama muendelezo wa Apple kuboresha bidhaa zao kwani hivi karibuni wametoa toleo jipya la AirPods ambazo zimewekwa kipuri cha H1 kinafanya iwe uwezo mkubwa wa kutunza chaji, mawasiliano mazuri kati ya vifaa, programu ya Siri iliyo bora zaidi.

Beats Earbuds zitauzwaje?
Kiuhalisia kabisa tusitegemee kuwa zitakuwa bei nafuu kwani sote tunafahamu bidhaa za bidhaa za Apple na kwa mujibu wa nyanzo mbalimbali bidhaa hiyo itauzwa kati ya $200-$250 ambazo ni zaidi ya Tsh. 460,000-Tsh. 575,000. Upande wa pili AirPods ni $160|zaidi Tsh. 368,000 na AirPods zenye teknolojia ya kuchaji bila waya ni $200|zaidi ya Tsh. 460,000.
Apple wanaendeleza wimbi la ushindani kwa wapinzani wao kwa bidhaa kama hizo kutoka Samsung, Huawei na Xiaomi. Vipi wewe ni mpenzi wa bidhaa za Beats? Basi jiandae kifedha ili kuweza kununua bishaa hiyo mpya inayotazamiwa kutoka mwezi Aprili.
Vyanzo: HypeBeast, GSMArena