EaseUS Data Recovery ni programu ya bure inayokusaidia kutafuta, na kuchagua kurudisha hai mafaili uliyokwisha yapoteza kwa njia kama vile kufuta bahati mbaya, kuformat diski zako (HDD, USB Flash Drive) n.k.
Tulishaandika kabla makala kuhusu – Jinsi Ya Kufufua Mafaili Yaliyofutwa Katika Simu au Kompyuta katika makala hiyo tuligusua zaidi programu kutoka kampuni ya Asoftech na muda huu tunaangalia jinsi ya kufanikisha jambo hilo hilo kupitia programu ya kisasa zaidi ya EaseUS Data Recovery kutoka kampuni ya EaseUS.
Asoftech Data Recovery kama uliijaribu ilikuwa inakupa uwezo wa kujaribu tuu – zaidi ya hapo lazima ulipie. Kwa EaseUS Data Recovery ni bure kuokoa (recover) data hadi GB 2 Bure.
Programu hii inaweza kuokoa aina zote za mafaili yaliyopotea, hii ikiwa ni pamoja na picha, document, video, mafaili ya sauti (nyimbo, n.k), na mafaili ya aina nyingi.
Kupitia programu hiyo unaweza okoa mafaili kutoka kompyuta, laptop, ‘hard drive’ – (SSD, HADD, USB nk), na vifaa vingine kama vile simu na tableti pale unapoziunganisha na kompyuta yenye Ease US Data Recovery.
Iwe faili limefutwa bahati mbaya, limefichwa, au kupotea kwa aina yeyote katika diski yako. Utaweza kuiokoa.
Idadi nzima ya mjumuisho wa ukubwa wa data unazoweza ku’recover hauna kikomo ila kwa toleo la bure unaweza kurudisha hai mafaili ya hadi GB 2. Hii ni tofauti na programu tuliyoiangalia mwanzo, ya Asfotech ambayo uwezi kurudisha hai mafaili yeyote bila kulipia.
Ukifungua programu mara ya kwanza utaona umeambiwa kuna 500MB za bure kuokoa, ila kwa kitendo cha kushare kwenye mitandao ya kijamii moja kwa moja kutoka programu hiyo unapata GB 1.5 ya zaidi.
Utumiaji
Ukishapakua na kufungua programu hii mara ya kwanza utaona sehemu inayokupa nafasi ya kuchagua aina ya mafaili unayotaka kuyarudisha hai (recover). Pia utaweza kuchagua ni diski (drive) gani unataka kuokoa data zako, kama ni diski ya USB (Flash Drive, HDD n.k).
Baada ya hapo utapata matokeo na utaweza kuchagua mafaili unayoitaji ku’recover.
Je umekwishatumia programu yeyote kwa ajili ya kuokoa mafaili uliyokwisha yafuta (delete/format)? Tuambie ulitumia programu gani kufanikisha kupata data zako?
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Mbunifu na mpenda teknolojia.Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri(at)teknokona.co.tz |