BBC imezindua huduma mpya ya umma ya kiteknolojia inayotoa taarifa za afya kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kupitia kwa programu ya kijamii ya kutuma ujumbe mfupi kwenye internet ya ‘WhatsApp.’ Programu hio inawalenga zaidi watumiaji wa Internet katika kanda ya Afrika Magharibi. Huduma hio itawezesha wasomaji kupata taarifa kwa njia ya sauti, ujumbe mfupi na picha kuwasaidia kuepukana na maambukizi ya Ebola katika kanda nzima.
Taarifa zitakazopatiakana kwenye App hiyo zitakuwa angalau tatu kwa siku na huduma yenyewe itakuwa kwa lugha ya kiingereza na kifaransa. Ili kupata taarifa kupitia kwa programu hiyo, tuma ujumbe mfupi…kupitia kwa WhatsApp kwa nambari +44 7702 348 651. ~BBC Swahili
Kwa mtazamo wangu uamuzi huu kwa BBC ni jambo zuri sana na lilitakuwa kufikiriwa na Serikali na wizara za afya za nchi hizi mapema zaidi. Ni mategemeo yetu watafanikiwa sana katika hili. BBC wanastaili hongera kwa uamuzi mzuri huu, mitandao ya jamii inazidi kushika kasi!!!
Je unafikiri kujiunga pia?
No Comment! Be the first one.