Microsoft Edge ni moja kati kivinjari maarufu sana na ni moja kati ya kivinjari chenye watumiaji wengi sana.
Kivinjari hiki kimekua kikijiboresha mara kwa mara na hivi sasa kinakuja na uwezo wa kuhariri picha kabla ya kuzishusha katika kifaa chako (kompyuta).
Hii yote inatokea huko mtandaoni, yaaani ukiwa unaingia katika eneo la kuhifashi picha (save) unaweza uki ‘Right Click’….
….kisha ukaona chaguo la ‘Edit Image’ ukichagua hapo basi ukurasa wa kuhariri utafunguka, sio kazi kubwa sio?
Hapo unaweza ukahariri picha hiyo jinsi unavyotaka kulingana na vipenfele ambavyo vipo. Kumbuka hakutakua na ugumu wakatika wa kutumia vipengele hivi kwani vingi vyao vinafanana kabisa na vile vya Windows 10 na 11.
Ili kufurahia huduma hii itakubidi kabisa uwe na toleo jipya kabisa (updated) la Microsoft Edge Canary Chanel ambalo ni toleo la majaribio la vipengele mbali mbali vya kivinjari hicho
Ndio, kwa sasa ni majaribio tuu lakini kuna hati hati kubwa sana baadae utaweza kutumia kipengele hichi katika kivinjari cha Edge kwa kawaida tuu.
Microsoft Edge Canary Channel Inapatikana >>HAPA<< …Au unaweza kusubiria mpaka kivinjari hicho kuanza kupatikana kwa watu wote.
Sio mara ya kwanza kwa kivinjari hiki kuja na maboresho au vipengele vipya kadha wa kadha na hii yote ni katika kujihakikishia kuwa inabaki katik nafasi za juu kati vile vivinjari bora.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hili umelipokeaje? Unadhani utakua mtumiaji mzuri wa kipengele hichi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.