Mfumo wa World Wide Web umefikisha miaka 21 wiki wii, na kwa wale wasiomjua aliyekuja na teknolojia hii ni Tim Berners-Lee, 41.
Na katika kitu cha ajabu mtu huyu ambaye angeweza kuwa mtu mmoja tajiri sana duniani ni kwamba anaishi maisha ya kawaida sana kwani hakujimilikisha teknolojia hii mwaka 1992. Na kitu kingine kuhusu yeye ni kwamba anachukia takribani ya asilimia 50 ya jinsi mtandao huu ulivyo siku hizi.
Anaishi maisha ya kawaida na anapinga mambo yote ya kutaka serikali kufuatilia au ku’control’ utumiaji wa teknolojia hii.
Ingawa teknolojia aliyoiingiza ndiyo inajulikana na kutumika na watu wengi zaidi jina lake halijapata umaarufu anaostahili. Huyu ndio Tim Berners-Lee!
Kwa mengi zaidi kuhusu yeye unaweza kusoma makala hii ya gazeti la Times iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza.
No Comment! Be the first one.