Elon Musk kutoa zawadi ya dola milioni 100, ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 230 kwa mtu au kampuni itakayokuja na teknolojia za kupunguza gesi za kabonidioksidi kutoka kwenye uso wa dunia.
Bwana Elon ametoa ofa hiyo kupitia akaunti yake ya Twitter alhamisi wiki hii, kwa maneno yake amesema anatoa zawaidi kwa atayekuja na teknolojia bora zaidi ya kupunguza gesi za kabonidioksidi.

Teknolojia hiyo imeanza kuonekana inahitaji kwa haraka zaidi kama ulimwengu unataka kufikia malengo ya kutoongeza gesi hiyo kwenye anga. Ingawa gesi hii ni muhimu ila shughuli za kibinadamu hasa hasa zinazohusisha viwanda zimekuwa zikiongeza gesi hiyo kwa kasi zaidi kuliko utumiaji wake. Jambo hili linachangia katika kusababisha mabadiliko ya hali ya hewa yaliyo maaribifu – kwa uchumi na afya za binadamu na viumbe vingine.
Elon Musk ni mkurugenzi mkuu katika makampuni yanaliyokuja na teknolojia za kisasa sana kwenye magari kupitia kampuni ya Tesla – magari yanayotumia umeme na yenye teknolojia za kujiendesha yenyewe, pia teknolojia ya kisasa katika safari za anga kupitia kampuni ya SpaceX.
No Comment! Be the first one.