Bwana Elon Musk, mmiliki wa mtandao wa kijamii wa X, uliokuwa unafahamika kwa jina la Twitter, amesema wanaangalia uwezekano wa kuondoa uwezo wa watu ku’block watumiaji wengine kwenye mtandao huo wa kijamii.
Jambo limepokelewa kwa utofauti na aina tofauti ya watumiaji wa mtandao huo, huku wengine wakiufurahia na huku wengine wakiona ni jambo baya ambalo linazidi kuonesha maamuzi yanayofanywa na Elon Musk yamekuwa ni ya ghafla yasiyochukulia kwa uzito masuala ya usalama kwa watumiaji wake.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na aina tatu za kuvunja uhusiano na watu unaowafuatilia au wanaokufuatilia kwenye mtandao huo.
- Ku’unfollow – kuacha kuifuatilia akaunti
- Ku’block – maarufu kama ‘kumtupia mtu tofali, hii inafanya mtu huyo kutoweza kuona akaunti yako au kile anachokiweka kwenye mtandao huo wa kijamii. Ukimblock mtumiaji ata wewe pia hautakutana na vitu anavyoviweka kwenye mtandao huo. Ingawa kumekuwa na njia ya kuiona akaunti husika au ata baadhi ya vitu kama utakuwa haujalogin ila bado njia hii imekuwa salama kwa watu ambao wamechukizwa na usumbufu au aina ya maudhui ambayo mtu mwingine anayaweka kwenye mtandao huo. Aliyepigwa tofali ni rahisi kugundua kama amepigwa tofauli kwani naye atashindwa kuona akaunti au maudhui ya mtu aliyempiga tofauli.
- Ku’mute – Kumute, ni kuzima mambo yote yanayohusiana na akaunti ya mtu flani, kwa kuyazima ina maana hayataoneshwa kwako. Njia hii inafanya pia mtu aliyepigwa tukio la kuzimwa kutoweza kufahamu kama mtu flani amechukua hatua hizo dhidi yake. Ni ya usiri. Aliyepigwa ‘mute’ bado anaweza kuona maudhui ya yule mwingine kama kawaida.
Block is going to be deleted as a “feature”, except for DMs
— Elon Musk (@elonmusk) August 18, 2023
Elon Musk anasema uwezo wa kumute unatosha na anaona suala la kupiga tofali si la lazima kuwepo.
Wengi wanatofautiana naye hasa wakisema uwezo huo unasaidia sana katika hali ya kuepusha usumbufu kutoka kwa watu ambao hutaki kuwa na mahusiano nao katika mtandao huo wa kijamii. Pia kuna uwezekano kama wakichukua hatua hiyo watakuwa wanavunja taratibu zilizowekwa na Google na App kama moja ya hitaji/sifa ya app ya mtandao wa kijamii kuwepo kwenye masoko yao ya apps. Hii inamaanisha uamuzi huo ukitelekezwa masoko hayo ya apps yatakuwa huru kuondoa app hiyo kutoka kwenye masoko yake.
Kuna wanaosema Elon anajali tuu ukuaji wa mazungumzo katika mtandao huo wa kijamii, bila kujali mazungumzo hayo kama ni mazuri au ni ya chuki na ugombanishi.
Vipi wewe unatumia mtandao wa X? Unauonaje uamuzi huu wa Elon Musk? Bado X hawajasema kama mabadiliko haya yatafanyika kweli au Elon Musk aliadhisha mazungumzo haya ili kuweza kupokea maoni mengi zaidi ili kuona kama watumiaji wake bado wanataka ‘uwezo wa kupigana tofauli uendelee kuwepo’.
No Comment! Be the first one.