Mmiliki wa Twitter bw. ELon Musk ameweka wazi kwa hadhira kwamba mtandao wa kijamii wa WhatsApp unachukua taarifa za watu bila idhini kwa kupitia kinasa sauti.
Taarifa hizo zinachukuliwa na mtandao wa WhatsApp kwa njia ya kinasa sauti (microphone) ambacho kipo katika simu ya mtumiaji na hii imetokea kwenye simu ya mfanyakazi wa twitter.
Elon musk nae ameonekana akilithibitisha hilo baada ya ku’tweet katika ukurasa wake wa Twitter na kuibua tahaluki kwa wafuasi wake na watu wengine.
Kinachoonekana hapo ni kwamba WhatsApp walitumia kinasa sauti cha simu ya mfanyakazi huyo wakati akiwa amelala –wakati hatumii kabisa kifaa hicho (mtandao huo).
Hiki ndicho ambacho kimeamsha maswali mengi na watu kuanza kujiuliza pengine mtandao huo unaweza ukawa unadukua taarifa za watu ambazo zinatakiwa kulindwa kwa hali na mali.
Kwa upande wa WhatsApp wao walikanusha kabisa taarifa hizo –kwamba hakuna anaedukuliwa—na kwamba hilo linatokana na sababu za kiufundi tuu ambazo zimepelekea jambo hilo na liko katika baadhi ya simu za Android tuu.
Mfanyakazi wa Twitter yeye alitweet na kusema kwamba “Twitter imekua ikitumia kinasa sauti cha kifaa change wakati nimelala na tangia nilivyoamka saa kumi na mbili asubuhi (na hii sio mara moja) nini kinaendelea??”
WhatsApp cannot be trusted https://t.co/3gdNxZOLLy
— Elon Musk (@elonmusk) May 9, 2023
Pande zote mbili zimejielezea kwa kina huku mtandao wa WhatsApp ukikanusha vikali kwa kusema kuwa ni tatizo la kiufundi (bug) tena pengine linaweza likawa katika kifaa cha mfanyakazi huyo tuu – Goole Pixel
Ningependa kusikia kutoka kwako niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani mtandao wa WhastApp haupo salama kama wafanya kazi hawa wa Twitter wanavyodai?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.