Emirates itakua ikishikilia mikoba ya kuwa ndege yenye safari yenye ruti ndefu zaidi duniani kutokana na huduma yake ya safari kutoka Dubai mpaka jiji la Panama. Safari hii itakua ni ya moja kwa moja. Huduma hii inategemewa kuanzishwa rasmi mwezi januari
Safari hiyo itakuwa na urefu wa kilomita 13,821 ambazo ni maili 8,590 ambazo pia ni kilomita 17 (maili 10.56) zaidi ya ile ambayo itakua ruti ndefu ya ndege katika nafasi ya pili. Ruti ya safari hiyo ni kutoka Sydney mpaka Dallas kwa kutumia ndege za Qantas.
Kwa Ruti hizo za anga Emirates itatumia ndege ya Boeing 777-200LR, ambayo pia safari yake itachukua takribani masaa 17 na dakika 35, Kampuni hiyo ya ndege (Emirates) ilisema
Pia ruti hiyo ya dubai mpaka jijini panama haitaweka rekodi kwa sababu kulikua na ruti defu zaidi ya ndege iliyokua ikimilikiwa na Singapore (Singapore Airlines). Ndege ilikua ikichukua abiria kutoka Singapore na Newark, New Jersey takribani kwa zaidi ya umbali wa kilomita 15,344 ambazo ni maili 9534.32 na ilikua ikichukua masaa 19 tuu.
Sasa jiji la Panama litakua ndio geti la wageni (Wanaotumia ndege ya Emirates) kuingi Amerika ya kati, Kaskazini kusini na hata pande zingine. Kutoka kwa mwenyekiti wa ndege hizo (Emirates) amesema kuwa pia ruti hiyo itasaidia katika uwezo wa bidhaa zinazoingia kutoka njee ya nchi kama vile elektroniki, bidhaa za mashine na hata madawa (ya matibabu)
Ndege ya Boeing 777-200LR kwa ruti hiyo itakua na siti 266 kwa jumla. Mpaka sasa Emirates ruti yao kubwa ni kutoka Dubai mpaka Los Angels ambayo ina umbali wa kilomita 13,420 (maili 8338.8) na inatumia ndege aina ya Airbus A38- superjumbo.
No Comment! Be the first one.