Je umeshawahi kutambua ya kuwa unaweza kuandika na kutafuta neno la jambo au mtu flani au chochote kile kwenye mitandao ya utafutaji (search) kama vile Google, Bing na Yahoo na bado utapata majibu tofauti kimpangilio? Tumia EML Search
EML Search ni tovuti ambayo ina uwezo wa kuleta matokeo mengi zaidi katika utofautaji kutoka mitandao yote mikubwa kama vile Google, Yahoo na Bing yote katika ukurasa mmoja na hivyo kukuonesha utofauti mkubwa katika matokeo kutoka mitandao hii maarufu.
Matokeo hayo ni pamoja na ata ya picha. Utaweza kuona utofauti ulivyo kutoka mitandao yote mitatu kwenye ukurasa mmoja.
Faida?
Wazo ni kuwezesha watumiaji wa kawaida kama vile watafiti, wanasayansi, wahandisi, madaktari, wanafunzi, wahandisi wa programu, wanabaiolojia, wasanii, watendaji, kutoweza kukosa vitu muhimu pale wanapotafuta vitu kwenye mtandao na kuwalazimu kutembelea mitandao yote mitatu tuliyoitaja. Kwa sasa kwa kutembelea EMLSearch utafanikiwa kupata matokeo kutoka mitandao yote mitatu mikubwa kwa wakati mmoja kwenye ukurasa mmoja. Hii itaokoa muda sana.
Pia utaweza kutuma matokeo uliyoyapata kwa rafiki au mtu mwingine yeyote kupitia barua pepe.
Unaweza kutembelea mtandao huu kwa kubofya hapa – http://www.emlsearch.com , pia unaweza ungana nao kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook –
Facebook: https://www.facebook.com/eml.web.search
No Comment! Be the first one.