Unicode ambao ndio wanahusika katika kuweka mwongozo wa utengenezaji wa emoji wametoa orodha ya emoji mpya 72 ambazo zitatolewa katika toleo jipya la unicode 9.0 ambalo litatoka tarehe 21 mwezi wa sita mwaka huu.
Unicode ndio wanaotawala sheria zinazotumika kutengeneza emoji duniani na kwamba makampuni kama vile Apple na google wanapokea design kutoka unicode na wanatengeneza emoji kutegemea sheria hizo.
Video kutoka Emojopedia ambayo inaelezea emoji zote.
Kila mwaka muungano huu hukaa na kutoa muongozo juu ya emoji kadhaa ambazo zimeonekana zinahitajika kutoka kwa watumiaji, mwaka huu wamekuja na muongozo wa kutengeneza emoji mpya 72 ambazo makampuni kama Apple na Google yatazipata na kuanza kuyafanyia kazi katika matoleo yao yajayo.
Emoji hizi ambazo zitanza kutumiwa tarehe 21 Juni (Tarehe hii ni ile ambayo makampuni kama Apple na Google watapata emoji hizi) na kwa sisi watumiaji wa kawaida itatuchukua muda kidogo mpaka kuzipata katika simu zetu. Wanaotumia vifaa vya Apple huenda watapata emoji hizi mapema zaidi kutokana na mfumo ambao Apple hutumia kupeleka matoleo mapya ya iOS.
Katika emoji hizo mpya 72 ni pamoja na ile ya mtu akicheka na kugalagala chini, uso ukiwa na kofia ya Cowboy, uso wa mwanamazingaombwe, uso wa mtu mwongo, uso wa mtu akitokwa udenda na nyinginezo nyingi.