Kampuni ya nchini Ufaransa, ya Avenir Telecom, imetambulisha simu ya Energizer Power Max P18K Pop, simu yenye uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu zaidi.
Simu janja hii inakuja na betri la uwezo wa mAh 18,000, kwa wastani simu nyingi huwa na kiwango cha betri cha kati ya mAh 2,500 hadi mAh 4,000. mAh – ni kipimo cha uhifadhi chaji/umeme wa betri za simu.
Kiwango hichi cha uhifadhi wa betri unafanya simu janja hii iweze kuwa na sifa kadhaa;
- Unaweza kusikiliza zaidi ya masaa 100 ya muziki
- Unaweza kutazama video kwa masaa 48 mfululizo
- Kwa watumiaji sana wa simu basi kwa kuchaji mara moja unaweza kuitumia wiki nzima bila kuchaji tena
Uwezo huu wa chaji unakuja na hasara moja tuu – HII SIMU NI NENE SANA. Kwa wastani unene wake ni sawa na kuziweka iPhone za kasasa tatu na nusu – ndio unapata ukubwa wa unene wa simu hii. Hii ikiwa ni unene wa mm 18.
Sifa zingine;
- Kwa nyuma ina kamera tatu, za MP 12, 5, na 2. Wakati kwenye selfi inakuja na kamera mbili, ya MP 16 na MP 2.
- Display ya inchi 6.2 (LCD)
- Inakuja na RAM ya GB 6 na diski uhifadhi wa GB 128
- Prosesa ya Mediatek Helio P70
- Programu endeshaji ya Android 9.0 (Pie)
- Redio (FM)
- Teknolojia ya Wifi,
Ubaya pia ni kwamba na ukubwa wake wote watengenezaji wameona wasiweke eneo la waya kwa ajila ya earphones. Imbidi mtumiaji atumie earphone za bluetooth.
Uwezo wa kuchaji kwa kasi ya haraka (fast charge), na pia uwezo wa kuchaji simu nyingine na hivyo kueguka powerbank.
Simu hii itakuja kwenye matoleo ya rangi ya blu na nyeusi.