Facebook ndio mtandao wa kijamii nambari moja duniani. Kuwa namba moja sio kitu cha mchezo hivyo inahitaji au inabiidi kufanya mambo mengi na ya kipekee ili kubaki hapo (namba moja). Mpaka sasa facebook ina vipengele vingi vya kipengee ambavyo hata nikianza kuvitaja sitavimaliza
Licha ya kuwa namba moja bado wanaendelea kuboresha huduma zao. Katika App yao ambayo ipo miongoni mwa App za kijamii ambazo zinaongozwa kushushwa duniani kuna mabadiliko yanafanyika ili kukuwezesha kuweza ku ‘comment’ katika post au picha hata ukiwa ‘offline’. Hii imelengwa kwa mataifa maskini (yale yenye shida ya intaneti) sana sana.
Lakini si hivyo tuu hata mataifa ambayo yameendelea kuna baadhi ya sehemu inakua ngumu kupata huduma ya intaneti mfano katika mahandaki au hata zile barabara za chini. huduma hii itasaidia yote hayo ingiwa imejikita katika nhi ambazo zina matatizo ya intaneti (nchi zinazoendelea)
Sasisho jipya hilo pia litakuwa na msaada sana kama intaneti ya mtumiaji itakuwa chini kwa wakati huo ambao anatumia kifaa chake kwani itamuwezesha kufanya mambo ya aina yake.
App ya facebook kwa kawaida huwa inakusanya (load) taarifa wakati kuna huduma ya intaneti nzuri na kisha inazihifadhi. Ukiingia inafanya tuu kukuonyesha ndio maana muda mwingine unaona habari hata za jana ziko kwa juu juu tuu katika App yako ya Facebook.
Ni kitu cha kipekee fikiria wakati una intaneti ya kutosha App inadownload taarifa za kutosha ambazo unaweza zisoma hata kama ukiwa hauna huduma ya Intaneti.
Katika maboresho haya yatawasaidia watumiaji wake wa nchi nyingi za Afrika kwani huduma ya intaneti bado ni gumzo. Saa zingine watu huwa wanataka kuingia katika mtandao huo lakini tatizo ni intaneti (mb 8). Hongera kwa Facebook kuliona hilo.
No Comment! Be the first one.