Facebook ni moja kati ya mtandao wa kijamii mkongwe kabisa na wenye watumiai wengi zaidi kwa siku.
Mara kwa mara mtandao huo wa facebook umeonekana ukiwa unabadilisha nembo yake mpaka kufikia hii ya sasa, na kwa sasa hakuna mabadiliko makubwa.
Unaweza ukawa unajiuliza kwanini mtandao unapitia mambo yote hayo, ila inakuaga ni sehemu tuu ya mabadiliko ili mradi tuu kuendana na hali halisi ya sasa.
Ni wzi kwamba mabadiliko haya sio makubwa sana maana ni katika swala la rangi tuu, nembo bado ni ile ile ilakilichobadilika ni swala zima la rangi tuu.
Inafahamika dhahiri kwamba logo ya facebook ni herufi ya ‘f’ ambazo imezungukwa na duara ambalo lina rangi ya bluu.
Kwa upande mwingine hili ni jambo jema kabisa maana kwa haraka haraka kampuni haijaamua kubadili nembo nzima bali katika swala la rangi tuu.
Kumbuka facebook kwa siku tuu wana watumiaji zadii ya bilioni mbili, hii ni namba kubwa sana ukilinganisha na mitandao mingine ya kijamii.
Kwa namba hiyo ingekua sio sawa kubadilishiwa tena nembo nzima ila swala la kubadilisha rangi katika nembo hiyo ni sawa tuu.
Nembo (Logo) Ambazo Facebook Wamewahi Kutumia Ni Hizi Hapa
Meta wao wameweka wazi kwamba kuna mabadiliko kadha wa kadha ambayo wamesema wanategemea kuyafanya katika mtandao huo lakini kwa sasa ni hayo tuu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je kama nisingekuambia kama nembo imebadilika ungeweza kugundua mwenyewe? Au TeknoKona ndio inakutonya?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.