Facebook na WhatsApp ni mitandao ya kijamii ambayo ni mikubwa na yenye majina makubwa sana duniani. Ikumbukwe kuwa FB ndio inaimiliki WhatsApp baada ya kuinunua miaka kadhaa iliyopita.
Facebook iliinunua WhatsApp lakini baadhi ya wafanya kazi na waanzilishi walibakia katika kampuni. Baada ya muda kidogo kulianza kutokea tofauti za kiuongozi na kimaono, hali ambayo imepelekea waanzilishi hao kujivua na kampuni ya WhatsApp. Hii sio mbaya sana kwani waliuza kampuni hiyo kwa FB kipindi cha nyuma.
Vile vile Facebook ilitangaza kuwa itaanza kurusha matangazo (ya kulipwa) katika mtandao wa WhatsApp kupitia eneo la status. Hii ikiwa ni njia moja ya kwa Facebook kujihakikishia kuwa wanaongeza pato lao
Facebook vile vile walitangaza kuwa WhatsApp na FB ziwe na daraja ambalo linaunga mitandao hiyo miwili, japokuwa wazo hilo lilipigwa na wengi lakini bado lilifanikiwa. Sasa hivi unaweza post status WhatsApp na Facebook kwa wakati mmoja.
Licha ya hivyo inasemekana kuwa FB inajikita zaidi katika kuhakikisha watu wenye biashara zao kupitia mitandao hiyo wanakutanishwa vizuri na kwa ukaribu zaidi na wateja zao na jinsi ya kusimamia mawasiliano/mahusiano hayo.

KWA TAARIFA YAKO
- Jarida la Wall Street limechapishwa kuwa timu ambayo ilibidi ifanye mchakato mzima imefutwa
- Ile ‘Code’ ambayo waliiandika WhatsApp ili ifanye zoezi hili imefutiliwa mbali
Sawa plani za FB kutangaza kupitia WhatsApp pengine inaweza ikawa ndio tamati, lakini ambacho kinajilikana ni kwamba WhatsApp bado inatafuta njia ya kuweza kutangaza kupitia katika eneo lake la status.
Soma Zaidi Kuhusu Facebook/WhatsApp