Facebook imetangaza kwamba itafanya mabadiliko katika mfumo wa sera yake unaowataka watumiaji kuthibitisha uhalisia wa majina yao wanayoyatumia katika mtandao huo. Hii itawasidia wale wote walioondolewa Facebook kwa kushindwa kuthibitisha uhalisia wa majina yao katika Facebook wiki kadhaa zilizopita.
“Watumiaji wa mtandao wa Facebook sasa wataweza kutumia majina ‘Feki’ kama hawatakuwa huru kutumia majina halisi katika mtandao huo.”
Mtandao huo, unafanya mabadiliko ya sera yake ya ‘Majina Halisi’ ili kuwawezesha watumiaji wa Facebook kuweza kutumia majina ‘feki’ tofauti na majina yao halisi katika mtandao huo.
Sera iliyopo inamlazimisha mtumiaji kutumia jina lake la kuzaliwa, na wakati mwingine baadhi ya watumiaji wametakiwa kutuma nakala za vyeti vyao vya kuzaliwa ili kuthibitisha uhalisia wa majina yao. Sera hii inawia vigumu kwa baadhi ya watumiaji kuweza kutambua majina halisi na feki mtandaoni.
Hili limekuja baada ya makundi kadhaa ya watumiaji wa mtandao huo kukosoa vikali sera ya kutumia majina halisi katika mtandao huo, huku wakisema kuwa inahatarisha maisha kwa baadhi ya watumiaji ambao majina halisi ni hatari kuwa hadharani kutokana na asili ya kazi zao.
Mashirika kadhaa ya kutetea haki za binadamu yakiwemo yale ya Electronic Frontier Foundation, Human Rights Watch, na ACLU ya California yameshiriki kukosoa sera hii ya Facebook na wameunga mkono kwa kuandika barua za wazi kwa maofisa wa mtandao wa Facebook.
“Tunataka kupunguza idadi ya watu wanaolazimishwa kuthibitisha uhalisia wa majina yao Facenbook, wakati kuna watu wanawafahamu kwa majina hayo wanayoyatumia”. Ilisema sehemu ya ripoti iliyotolewa na afisa mkuu wa bidhaa kutoka Facebook, Chris Cox kujibu barua hiyo ya wazi.
Kufanya hivyo, wale watakaokuwa wanajisikia kutumia majina yanayoendana na mantiki fulani kuwafikia kundi fulani la watu sasa wataweza kufanya ivyo. Hawakuweza kufanya ivyo kabla.
Mabadiliko hayo yanatazamiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu.
Katika maelezo yake, Cox amebainisha kuwa lengo kuu la kutumia majina halisi ni kuwafanya watu wajue kuwa watahusika na lolote watakaloandika katika kurasa zao za Facebook, labda zinazohusiana na matusi, uonevu, virusi na kadhalika.
Chanzo cha Makala haya ni Chris Cox, Facebook na mtandao wa Fortune.
One Comment