Mkurugenzi mkuu wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckeberg ana plani kadha wa kadha na mtandao wake wa kijamii. Plani zake zinamuambia ifikapo 2030 Facebook itakuwa na watumiaji bilioni 5.
Pata picha mtandao wa kijamii, Facebook kuwakutanisha au kuunganisha watu bilioni 5 duniani. Habari hii imetangazwa na mkurugenzi huyo katika siku ya marafiki (siku ya kuzaliwa kwa FB) wa Facebook katika makao makuu ya ofisi hiyo. Sikukuu hii ilikuwa ya kusheherekea miaka 12 ya mtandao huu wa kijamii wa Facebook.
![](https://teknokona.com/wp-content/uploads/2016/02/mark-zuckerberg-facebook-will-add-35-billion-users-by-2030.jpg)
“Tunataka kumaliza kumuunganisha kila mtu, tunataka kufanya hivyo kwa kuungana na serikali pamoja na makampuni mengine kadha wa kadha duniani kote” – alisema Bw. Zuckerberg
Mpaka sasa Facebook ina watumiaji zaidi ya bilioni 1.5 na zaidi, hii inaonyesha ni jinsi gani mtandao huu wa kijamii ulivyoendelea kwa kuunganisha watu duniani.
Pia ukiangalia kuwa Facebook imekuwa kwa kiasi kikubwa bado inataka kuongeza watumiaji bilioni 3.5, kumbuka hii sio rahisi kihivyo lakini kwa kuboresha huduma na elimu juu ya mtandao huu wa kijamii lolote linaweza likatokea.
Kumbuka dunia sasa ina watu bilioni 7 na kumbuka pia katika watu hao kuna watoto wadogo ambao hawaruhusiwi kutengeneza akaunti za Facebook. Kwa hapa Facebook inatakiwa kuwafanya watu wazima tuu kujiunga katika mtandao huo.
Pia usisahau, hii ipo hivi kama watu hawataongezeka basi kwa miaka 14 ijayo Facebook itafikia watu bilioni 5 kama inavyokusudia. Wakiongezeka, watoto wakikua na watu wazima wakijiandikisha kwa wingi basi inawezekana hata idadi hii ikafikiwa kwa muda miaka michache ijayo.
Kutokana na taarifa za Umoja wa Mataifa (UN) zinasema kuwa idadi ya watu duniani itafikia mpaka bilioni 8.5 ifikapo 2030. Kwa kuunganisha haya mawili yote pamoja, Facebook inaweza dhahiri kuwa na watumiaji bilioni 5 katiki ya wale bilioni 8.5 kwa mwaka 2030 kama plani zao zikifaniwa.
Facebook ipo katika hatua ya kuhakikisha dunia nzima inaungana kupitia mtandao wake katika kipindi cha muda mchache tuu. Kumbuka wana mpaka mpaka huduma ‘Free Basics’ ambayo inawawezesha watu kuingia katika mtandao hata kama hawana vifurushu vya intaneti au salio katika simu zao.
No Comment! Be the first one.