Facebook wameongeza taarifa mbalimbali ambazo zitawawezesha watumiaji wa mtandao huo kwa kufuatilia na kuweza kutafuta bidhaa ambazo zitawavutia kutokana na mahitaji yao.
Hivyo hivyo Facebook wanatuma taarifa hizo kwa wenye biashara kutokana na taarifa yako kuhusu bidhaa zinazokuvutia.
>Jinsi mfumo huo unavyofanya kazi
GPS inatakiwa kuwa “on” kisha Facebook watafuta duka lenye bidhaa unazozipenda kisha kukutumia tangazo hilo. Ukivutiwa na tangazo na kwenda kutembelea duka linalouza bidhaa hizo Facebook watajua kuwa umetembelea duka hilo kutokana na tangazo walilokutumia.
Teknolojia hii sio mpya sana kwani mwaka 2014 Google nao walijaribu kufanya kitu kama ambacho Facebook wamezindua hivi karibuni ila kitu ambacho ni cha kipekee kuhusu hiki ni uwezo wa kufuatilia kwamba mataangazo ya bidhaa hizo yanaendana na mauzo ya bidhaa hizo.
Mbali na hilo Facebook wameongeza namna ya kuwaunganisha watumiaji wa Facebook na yale matangazo ambayo yanaongoza katika mauzo ya bidhaa zake na hivyo kuzidi kujiongezea mapato kati ya duka linalouza bidhaa hizo na Facebook kwa ujumla.
Pia, Facebook wameweka option ya “Store locator” kwenye matangazo ya biashara hizo itakayokuwezeshesha kufika kwa urahisi katika duka linalouza bidhaa hizo iwapo utakuwa umevutiwa na tangazo hilo kuhusu bidhaa fulani.

Ubunifu huu mpya haika utawaongezea Facebook pesa nyingi katika huduma za matangazo ila pia inaweza kuwauzi baadhi ya watumiaji wasiopendwa kufuatiliwa.
Niambie maoni yako kuhusu mbinu hii ya kibiashara kutoka Facebook kwa kuandika comment yako hapo chini. Je wapo sahihi kutufuatilia zaidi? Endelea kuhabarika kupitia mtandao wako wa Teknokona.
Chanzo: Extreme Tech, Vanity Fair Hive