Wiki hii Facebook imetangaza kwamba itajenga Kituo chake cha data cha pili ulaya katika mji wa Clonee nchini Ireland, hiki ni kituo cha pili Ulaya baada ya kile iliyojengwa Swedeen mwaka 2013.
Kituo hiki cha data kinatarajiwa kuanza kufanya kazi mwanzoni wa mwaka 2018 kama sio mwaka 2017 mwishoni, Facebook inasema kwamba kituo hiki pia kitatumia nishati mbadala kwa asilimia 100 kama ilivyo kituo kama hiki kilichojengwa mwaka 2013 huko Sweeden.
Kituo cha data ni nini!?
Wewe kama ni mtumiaji wa Facebook basi ni lazima katika ukurasa wako unaweka picha pamoja na status mbalimbali, vitu hivi unaweza kuvipata mda wowote unapotaka kuviangalia mfano nikitaka kuangalia picha yangu ya facebook niliyoweka mwaka 2008 nina weza. Bila shaka status na picha tunazopakia katika mtandao wa Facebook zinahifadhiwa katika server za mtandao huu, Ukubwa wa server za mtandao zinategemea ukubwa wa mtandao husika na Facebook ambayo inawatumiai zaidi ya milioni 900 basi ni mtandao ambao mkubwa na hivyo unahitaji server kubwa na nyingi zilizo katika mpangilio bora. Mkusanyiko wa server hizi ndio tunaita Kituo cha data.
Zipo changamoto kubwa nyingi katika ujenzi wa kituo cha data lakini changamoto za aina ya nishati inayotumika kuendesha mitambo pamoja na madhara ya kituo hicho katika madhingira ndiyo zinaangaliwa zaidi na ndio maana Facebook wameamua kutumia nishati mbadala katika kuendesha kituo hiki kipya kitakachojengwa karibu na mji wa Dublin.

Kituo hichi cha data ambacho ni cha sita kitatumia mfumo wa kupooza ule ule unatumia hewa ila hapa hewa hii itachujwa saana ili kuondoa chumvi chumvi. Pia miundombinu ya kituo hiki itakuwa imejengwa kutokana na mradi wa Facebook wa Open Compute Project.
Makamu wa raisi wa Operesheni wa Facebook Tom Furlong anasema kwamba kituo hiki kitajengwa katika teknolojia ya hali ya juu na kwamba kitakuwa katika ufanisi wa hali ya juu.
No Comment! Be the first one.