Facebook wanatarajia kuachia kitumizi kinachojitegemea kwa ajiri ya habari wiki ijayo, hii ni kwa mujibu wa habari za chini chini kutoka katika vyanzo vya kuaminika.
Kwa mujibu wa mtandao wa Financial Times Facebook wanategemea kuzindua kitumizi cha kujitegemea kitakachokuwa kinaitwa Notify kwa ajiri ya habari pekee baada ya kupata muitikio mzuri kutoka kwa watumiaji wake waliotumia huduma kama hii ambayo haikuwa ikijitegemea.
Notify itakuwa ni majibu ya facebook kwa mitandao mingine ya kijamii ambayo imepata umaarufu baada ya kujihusisha na habari, Snapchat kwa mfano wao walileta huduma ya Discover mwezi wa kwanza mwaka huu, huduma hii inakuwezesha kuona habari kutoka mitandao mikubwa kama CNN kwa urahisi na baadaye Twitter nao wakaleta huduma ya Moments (huduma hii bado haijatolewa kwa watumiaji wote) ambapo wao wanachomeka vibandiko vya habari katika ukurasa wako na kukufanya usome habari bila ya kwenda katika ukurasa wa habari husika.
Facebook na mitandao mingine inajikita katika ushirikiano na makampuni ya habari kwa kuwa matangazo ya ndani ya habari zao huwa yanalipiwa kiasi kikubwa cha fedha na hivyo kuifanya mitandao hii ya kijami kupata mapato zaidi. Facebook tayari wamekwisha tangaza kuwa zaidi ya robo tatu ya mapato yake yanatokana na matangazo, hivyo sio jambo la ajabu kuona jinsi wanavyo fanya mabadiliko na kuhakikisha wanapata makampuni mengi zaidi kuweka matangazo.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Facebook kuanzisha kitumizi kinachojitegemea, Messenger ni mfano wa mafanikio ya Facebook katika vitumizi vya kujitegemea. Ingawa pia yapo majaribio ya kuanzisha vitumizi vya kujitegemea ambayo hayakufanikiwa kama huduma ya Slingshot wacha tuwe na mtizamo chanya juu ya mafanikio ya Notify
One Comment