Mtandao wa Facebook umethibitisha kufanyia majaribio huduma mpya ya msadizi wa kidigitali aliyepewa jina la ‘M’ kama sehemu ya huduma ya Facebook Messanger. ‘M’, (uvumi unasema herufi hii inasimama badala ya maneno “Moneypenny”, msaidizi katika filamu za James Bond) itakua inafanya kazi kama huduma ya Apple ya ‘SIRI’ au ile ya Android ya ‘Google Now’.
Misingi mikuu ya Facebook M ni kumtafutia mtumiaji maelezo binafsi, kununua baadhi ya vitu na huduma kwa ajili yake, kuweka ahadi, kupeleka zawadi kwa wapendwa, na vyote hivi vinasaidiwa na huduma za kiautomatiki zinazofuatiliwa kwa karibu na watu wa kawaida.
Huduma hii itajumuisha akili za wasaidizi wa kiautomatikia pamoja na za watu wa kawaida katika baadhi ya matakwa. Sasa inafanyiwa majaribio katika baadhi ya watu katika jimbo la San Fransisco huku baadhi ya wafanyakazi wa Facebook wakiwa wamethibitisha kutumia huduma hiyo.
Misingi mikuu ya ‘M’ ni kumtafutia mtumiaji maelezo binafsi, kununua baadhi ya vitu na huduma kwa ajili yake, kuweka ahadi, kupeleka zawadi kwa wapendwa, na vyote hivi vinasaidiwa na huduma za kiautomatiki zinazofuatiliwa kwa karibu na watu wa kawaida.
Baadhi ya picha zilizotolewa na Facebook, zinaonyesha huduma ya ‘M’ ikiwa kazini, huku ikimuwezesha mtumiaji kuuliza aina ya vyakula vya kutumia katika miji tofauti, wapi pa kupitia chakula, na hata kuagiza ‘M’ kukuwekea oda ya chakula katika migahawa inayouza chakula hicho.
Huenda huduma hii ikawa mbioni sana kutoka, japo Facebook hawakusema tarehe hasa ya kuachiliwa kwa ‘M’.
Watumiaji wa Messenger duniani kote, wamekua wakiongezeka kila mwezi hadi kufikia milioni 700 kama mwanzilishi wake Mark Zuckerberg alivyojulisha mapema mwaka huu.
Soma Pia – Teknolojia: Simu Janja na Apps Zinawasaidia Watu Wenye Matatizo ya Kuona (Vipofu)
Baadhi ya waangalizi wamesema huenda ‘M’ ikapata Changamoto kama vile gharama za kuendesha na kutumia huduma hiyo, au suala la Kijiografia kwani si kila nchi duniani kote ina maeneo yanayotambulika na watu wote.
Una maoni gani juu ya teknolojia hii? Tungependa kusikia kutoka kwako.
No Comment! Be the first one.