Facebook wametangaza kuanza kuwezesha uwezo wa kupiga simu kwa watu wengi kwa wakati mmoja (Groups calls) kwa watumiaji wa Android na iOS ndani ya app ya Facebook Messenger.
Habari hiyo iliyotangazwa na mkuu wa Facebook Messenger bwana David Marcus kupitia mtandao wa Facebook utawawezesha watumiaji wa Facebook Messenger kupiga simu na kuwezesha mazungumzo ya watu wengi kwa wakati mmoja.
Kwa njia rahisi ya kubofya eneo la alama ya kupiga simu ndani ya kundi la watu unaochat nao mtumiaji ataweza kuwapigia simu wote waliokwenye kundi hilo kwa wakati mmoja….na hivyo kuweza kufanya mazungumzo kwa wote.
Uwezo huo wa kupiga simu umewekwa wa hadi kupiga simu kwa watu 50 kwa wakati mmoja, ili kuwezesha uwezo huu mpya katika app ya Facebook Messenger unatakiwa usasishe (update) app hiyo na kisha ndani masaa kadhaa utaweza ona uwezo huo ukiingia kwenye chat ya group.
Facebook wanazidi kuleta mapya ndani ya app ya Facebook Messenger kwani watu wengi bado wanaona ulazima wa kuwa na app hiyo haupo kwa sana. Na pia inaonekana Facebook wanalengo la kutaka kuwa app namba moja kwa ajili ya mawasiliano ya kila siku.
Je una mtazamo gani na teknolojia hii? Umeijaribu? Tungependa kusikia kutoka kwako.
Chanzo: FirstPost na mitandao mbalimbali