Facebook wanazidi kulazimisha watumiaji wake kupakua app ya Messenger katika simu zao. Katika uamuzi mwingine wa kuzidi kulionesha hilo wameamua kuondoa kabisa uwezo wa kuchati na marafiki katika toleo la tovuti hiyo linalopatikana kwenye simu.
Facebook Messenger ni lazima kuwa nayo….kama unaitaji kuchati na marafiki zako wa mtandao huo kwenye simu yako.
Uwezo wa kuchati kwa kutumia app ya Facebook Messenger ulianza kusukumwa kwa watumiaji pale ambapo Facebook waliondoa uwezo wa kuchati katika app yao ya Facebook. Kwa sasa hali ilivyo ni kwamba ukienda eneo la kuchati utaona tangazo la ku’download Facebook Messenger ila unaweza kulifunga na kuendelea kuchati…ila uwezo huu utaanza kuondolewa mara moja taratibu kwa watumiaji wote.
Wengi wanaona mabadiliko haya hayakuwa ya kiulazimu kabisa na si vizuri kulazimisha watu kupakua app wasioihitaji au kuona umuhimu wake kabisa.
Soma Pia- App ya Metal, Tumia Facebook bila simu kuishiwa chaji haraka zaidi
Kama wewe ni mtumiaji sana wa huduma ya kuchati katika mtandao wa Facebook basi utakuwa hauna budi bali kupakua app hiyo.
Je wewe una mtazamo gani juu ya suala hili? Unatumia app ya Messenger pia?
Facebook Messenger – Google Playstore | AppStore