Facebook mwishoni mwa wiki walifanya jaribio la kuongeza kionjo cha maua katika kitufe chake cha Facebook reaction kwa baadhi ya watumiaji kwa ajiri kusheherekea siku ya kinamama duniani.
Kitufe hiki cha maua kwa ajiri ya kuonesha shukurani kililetwa siku ya wanawake duniani kwa baadhi ya watumiaji wa Facebook katika masoko fulani duniani.
Kitufe hiki cha maua kuonesha shukurani kilikuwa maalumu kwaajiri ya siku ya kinamama duniani na hakitaendelea kuwepo kwaajiri ya kutumika baada ya siku ya wanawake lakini kwa wale waliobahatika kukitumia basi kitabaki katika post hizo hata baada ya siku hii ya kinamama.
Soma: Facebook reaction; Sasa facebooksa zaidi ya like, waleta emoji.
Kuwekwa kitufe hiki maalumu katika siku ya kina mama kinamaana mbili, moja ni kwamba pengine Facebook wataanza kubadili kitufe cha reaction kulingana na matukio maalumu kama vile siku ya wanawake nk.
Kama Facebook kweli wataanza kubadilisha Facebook reaction kulingana na sikukuu maalumu duniani basi watakuwa wamefuata nyayo za Google ambao wao hubadilisha doodle (ambazo ni picha za vikaragosi vinavyoonekana katika ukurasa wa google) kila katika sikukuu kubwa.
lakini hili jambo hili pia linaashiria kwamba bado kuna maboresho yatafanyika katika kitufe hicho cha Facebook reactions kuweza kuwasilisha hisia nyingine ambazo mabadiliko ya mwanzoni hayakuwa yamegusia.
Mwisho wa siku Facebook wanatafuta namna ya kuweza kupata watumiaji wapya zaidi na kuweza kuweza kuwa ni mtandao unaotumika zaidi, hii itawasaidia katika mapato kwa kuletewa mtangazo zaidi.