Ndiyo, hicho ndicho kilichotokea. Miezi kadhaa iliyopita Facebook walizindua huduma ya barua pepe ambayo hakuna watu walioishabikia sana kwani wengine hata hawakutambua uwepo wake, kwa maana bado watumiaji wa Facebook hawakuhamisha matumizi yao ya barua pepe kutoka huduma makampuni kama Gmail au Yahoo.
Sasa Facebook wamebadilisha anuani za barua pepe kwenye ‘Profile’ za watumiaji wake bila kutoa taarifa!
Ghafla Facebook wamebadilisha anuani za barua pepe katika ‘profile’ za watu kutoka anuani zozote ulizokuwa umeweka na kuweka ya @facebook.com kwa kutumia ‘username’ yako. Kwa mfano ‘username’ yangu ni stevpm hivyo wametoa anuani zangu zingine za barua pepe na kuweka moja ya stevpm@facebook.com.
Facebook wamelaumia sana kwa walichokifanya kwani hawajatoa taarifa yeyote. Na hakika kitu kama anuani ni kitu binafsi sana na hawakuwa na haki ya kukufanyia mabadiliko ya lazima.
Je jinsi gani ya kurekebisha?
Ukienda kwenye ‘Profile’ yako, bofya ‘About’, baada ya hapo utafunguka ukurasa wenye habari mbalimbali za ‘profile’ yako ambazo unaweza zifanyie mabadiliko (edit) za haraka hapo hapo.
Kwa hiyo nenda sehemu ya ‘Contact Info’ na bofya ‘edit’
Itatokea kitu kama hapo juu, sasa utaweza kuziona anuani zako zingine zilizofichwa hivyo pembeni yake unaweza fanya mabadiliko. Chagua nani ataweza kuona kama je ni marafiki au wewe mwenyewe tu, au kila mtu mwingine wa mtandaoni, chaguo ni lako.
Ukishamaliza kufanya mabadiliko uyapendayo usisahau kubofya ‘Save’, utaona mabadiliko kama ilivyotokea kwangu ambapo sikutaka barua pepe ya @facebook.com itokee.
BAADA YA MABADILIKO |
No Comment! Be the first one.