Facebook wameanzisha kipengele kipya Jumanne hii kinachoitwa Scrapbook, Ambayo inawezasha wazazi kutengeneza na kushare albamu (Za Picha) za watoto wao.
Scrapbook ni tofauti na kwa picha za kawaida katika facebook. Wazazi wana mamlaka ya kutoa vibali nani aone picha hizo na kivipi watag watoto wao. Wazazi tuu ndio watakua wanaweza kutoa mchango na mtu mwingine hawezi kutoa mchango wake isipokuwa kuona tuu hizo picha kama wazazi wataruhusu
Scrapbooks inapatikana katika facebook ya mtandao na hata katika App yake ya kwenye simu. Ili kupata kiengele hiki wazazi inabidi waorodheshe watoto wao kama watoto wao katika sehemu ya wanafamilia katika taarifa za mahusiano (Relationship information). Wanaomiliki wanyama wafugwao wa mapambo (pet) pia wanaweza tengeneza Album zao lakini inawabidi kuwaorodhesha hayo wanyama.
Facebook pia iliripotiwa kuwa na mpango wa kuwa na kipengele ambacho kitaweweza watoto kwenye Scrapbook kumiliki akaunti hiyo kipindi pale wanapofikia miaka 13 na wataruhusiwa kujiunga facebook wenyewe
Facebook bado hawajajua wataendesha vipi Scrapbook kwa familia zenye watu wengi kama vile watoto wa kambo, watoto wa mjomba n.k kwa sababu kwa sasa ni wazazi wawili tuu ambao wanaweza kutumia Scrapbook
No Comment! Be the first one.