Facebook imezindua kipengele kipya cha usalama kinachoitwa ‘Trusted Contacts’ ili iwe rahisi kwa watumiaji wa Facebook kuokoa akaunti zao pindi wanaposhindwa kwa sababu kama kusahau au mtu aliyeweza kujua taarifa zao za kuingilia kuzibadilisha (pia kwa njia maarufu ya ku’hack’).
‘Trusted Contacts’ ni huduma ya dharura kuwezesha marafiki zako kukusaidia kurejesha upatikanaji wa akaunti yako kama ni kuathirika na kuibiwa akaunti (hack) au kusahau taarifa zako kama ‘password’.
Facebook imeshauri kwamba unapaswa kuchagua watu wako wa karibu ambao unaweza ata kuwaamini na funguo za nyumbani kwako.
Mfumo huu utafanya kazi kama ifuatavyo;
1: Utachagua watu/marafiki watatu hadi watano unaowaamini
2: Pale utakaposhindwa kuingia kwenye akaunti yako (ku’log in’) badala ya kuwa na kazi ya kukumbuka taarifa flani flani kama zamani kwa sasa utaruhusu marafiki zako watumiwe namba za siri tofauti tofauti.
3: Utawasiliana nao wakupatie namba hizo, utaingiza namba hizo za siri na kisha utaweza kuingia kwenye akaunti yako.
HAPA CHINI NI MAELEZO YA JINSI YA KUWEZESHA ‘TRUSTED FRIENDS’ KWENYE AKAUNTI YAKO!
A: Ukiingia kwenye akaunti yako, nenda kwenye ‘Account Settings’
B: Kisha bofya sehemu ya ‘Security’
C: Utaona sehemu ya ‘Trusted Contacts’ kama inavyoonekana hapa chini
D: Bofya hapo na chagua watu 3 hadi 5 unaowaamini
E: Ukishawachagua Eneo la ‘Trusted Friends’ litabadilika
likikutaarifu idadi ya watu uliowachagua,
usihofu kwani utaweza kubadilisha watu muda wowote unaotaka.
Endelea kusoma teknokona.net , usisahau ku’like’ ukurasa wetu wa Facebook hapa na Twitter hapa.
No Comment! Be the first one.