Mtandao wa jamii mkubwa duniani wa Facebook umekuja na mambo mapya katika kuboresha zaidi mtandao huo. Kipya katika mtandao huo itakuwa uwezo wa watumiaji kuweza kuweka picha ambazo ni video fupi za takribani sekunde 7 zitakazoweza kujicheza mara moja mtu anapokuwa katika eneo linaloonesha picha ya ‘Profile’ ya mtumiaji.

Mtandao wa Facebook unawatumiaji zaidi ya bilioni 1.49 duniani kote, uwezo huu wa kuweza kutumia video fupi kama ‘profile picture’ umeanza kusambaa taratibu kwa watumiaji wachache kwa majaribio na utaendelea kusambaa kwa wengine wote.
Mabadiliko haya yanafanyika kwa ajili ya kuzidi kupendezesha mtandao huo kwa watumiaji wa simu za mkononi. Vingine vipya itakuwa ni pamoja na mabadiliko ya eneo la ‘profile picture’, litasogezwa kwenda katikati ya eneo la ‘coverphoto’.
Pia profile picha zitakuwa kubwa zaidi kulinganisha na muonekano wa sasa
Pia kingine kipya ni pamoja na uwezo wa mtumiaji wa mtandao huo kuchagua picha kadhaa azipendazo kuwa picha kuu za kwanza kuonekana katika eneo la profile yake.

Utaweza pia kuwa na picha za Profile za muda mfupi, yaani utaweka ‘profile picture’ ambayo utaipa muda wa kutoka (ku’expire). Picha hiyo itabadilika mara moja baada ya muda wake uliouchagua kuisha.
Kwa kiasi kikubwa mtandao wa Facebook unajitahidi kufanya mabadiliko makubwa ili kuzidi kuwavutia watumiaji wa mtandao huo kutumia muda mwingi zaidi katika mtandao huo.
No Comment! Be the first one.