Facebook sasa wameweka kipengele cha ‘Donate Now’ (Yaani changia sasa). Kipengele hiki kimeongezwa kikiwa na makusudi ya kusaidia watu au makampuni yanayohitaji msaada wa kifendha juu ya jambo fulani. Ingawa kipengele hichi kinajikita zaidi katika taasisi ambazo zipo kwa ajili ya kutoa huduma fulani (zisizo kwa lengo la kutengeneza faida)
Kila siku watu (biashara) zinatumia mtandao wa kijamii wa facebook kuongeza ujulikanaji wake, facebook wameliona hilo na wameamua kuweka kipengele hiicho ambacho kitasaidia taasisi hizo. Facebook inaelewa kwa kina jinsi watumiaji wa mtandao huo wanavyoweza kua watoaji wa msaada. Kitu kama hiki kilitokea hata baada ya tetemeko la ardhi huko Nepal. Michango kwa wakati huo ilionyesha umuhimu wake, baada ya siku tatu tuu baada ya kipengele hiki kutumika ilipatikana michango ya dola za kimarekani milioni 10.
Kitufe cha ‘Donate Now’ kinapatika pembeni kidogo ya kitufe cha ‘Like’ katika ukurasa wa taasisi ndani ya facebook. Mtumiaji wa facebook aki ‘click’ hapo atapokea ujumbe unaomuambia kuwa facebook haijuhusishi kwa lolote na taasisi hizo (zisizo za kujipatia faida). Baada ya hapo atapelekwa katika tovuti ya taasisi hiyo, mahali ambapo ataweza kukamilisha mchango wake.
Baadhi ya taasisi ambazo zinatumia kitufe hicho (Donate Now) ni ‘American Cancer Society’ na ‘The ALS Association’.Cha kushangaza ni kwamba kipengele hiki kilianzishwa tangia mwaka 2013 lakini taasisi chache ndio zilichaguliwa kukitumia. Taasisi hizo zilikua zikijumuisha DonorsChoose.org, Red Cross na UNICEF.
Sasa itakua ni tofauti kama ilivyokuwa mwanzoni ambapo watu walilazimika kutoa michango yao kupitia facebook moja kwa moja. Sasa itawabidi watoke nje ya facebook na kwenda katika tovuti ya taasisi husika na kisha kutoa mchango huo.
No Comment! Be the first one.