Vyanzo vya kupata habari zimekuwa ni vingi sana na kutokana na ukuaji wa habari ni wazi kwamba si kila habari (hasa za kutoka kwenye mitandao ya kijamii) ni za ukweli na imekuwa ni changamoto kwa kiasi chake kudhibiti habari ambazo hazina ukweli.
Katika juhudi ambazo Facebook ilizianzisha tangu mwaka uliopita (2016) baada ya kashfa ya kuwa na machapisho ya habari za uongo Facebook imekuwa ikionyesha jitihada mbalimbali katika kuhakikisha kuwa mtandao huo wenye watumiaji zaidi ya bil. 2 kwa siku unakuwa na habari ambazo ni za kweli tu.
Kipengele hiki (Trust Indicator) kitasaidia wasomaji kuweza kujua mengi zaidi kuhusiana na chanzo cha habari, miiko ya habari, mwandishi husika na pia kama habari yenyewe ni ya kuaminika.
Kipengele hiki kimewekwa kwenye ukurasa unaoongelea kitu fulani mathalani ukurasa wa TeknoKona kwenye Facebook.
Sekta ya habari na mawasiliano imekuwa katika wakati mgumu sana kwa kukabiliwa na kashfa mbalimbali kutokana na hekaheka za utafutaji wa habari ambazo nyingine zinakuwa sio za kweli jambo linalopelekea mhusika kusakamwa na mamlaka husika na hata kufungiwa kama funzo kwa wengine kile kilichotokea.
KIpengele hiki kinaweza kuwa moja ya silaha nzuri kwa mtu ukurasa wake kupata wafuatiliaji wengi kila siku kutokana na kile anachokichapisha kinatoka kwenye chanzo/vyanzo vya kuaminika na kutokana na ukweli kwamba Facebook ina watumiaji wengi basi ukurasa wa kweli utaona matunda yake kipengele hicho.
Vyanzo: The verge, PCMag, Fast Company