Maisha yetu yanazidi kuwa rahisi na hii yote inasababishwa na ukauji wa teknolojia, miaka ya nyuma ilikua ni ngumu sana kwa mtu kuweza kukopi maneno ambayo yapo katika picha.
Hii ni kwa watumaijia wa Android na iPhone (ios) tena kwa kutumia App yao ya Google Photos. Google Photos ni App mojawapo nzuri sana na inatumika katika kuhakikisha kuwa unasimamia picha dhahiri.

Hapa kwa kutumia huduma ya Google Lens ambayo inapatikana ndani ya App ya Google photos humo humo.
Sasa basi ili kutumia huduma hii ni lazima kuwa na picha ambayo ina maneneo ambayo unataka kuyanakili (copy), hii inaweza ikawa ni picha ya kitu chochote hata kama ni ‘Screenshot’

Hapo huna budi kufungua App hii na kisha chagua picha hiyo ambayo unataka kunakili maneno.
Ikishafunguka hapa yanaweza yakatokea mambo mawili, picha yenyewe ikaja huku maneno yakiwa yashajiwekea alama ya kujichagua tayari kwa ajili ya kunakili

Kama hilo halijawezekana basi unaweza kuingia katika sehemu ya Lens katika upande wa chini pale na kisha itajipeleka katika uchaguzi wa maneno hayo.

Ukiahamaliza uchaguzi kisha chagua ‘copy text from image’ ili kuweza kunakili maneno hayo.
Mpaka hapo nadhani unatua ushajua namna ya kulifanya hili jambo, Ningependa kusikia kutoka kwako niandikie hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.