Sahihi za Mkono za kwenye mtandao zimekua kwa kiasi kikubwa sana, mpaka sasa kuna hadi vifaa maalumu ambavyo vinaweza wezesha jambo hili
Ukiachana na vifaa hivyo, fikiria kama utakua una uwezo wa kuweka sahihi hizo ukiwa ndani ya Google Docs.
Kama umeshawahi kutumia huduma ya Google Drawings itakua ni rahisi Zaidi maana utakua huna haja ya kutengeneza sahihi (signature) mara mbili, kama bado haina shida
Fuata Njia Hizi Ili Kuweza Kulifanikisha Hili
Ili Kuanza ingia katika Google Docs, na kasha ingia kupitia account yako ya Google, katika eneo ambalo unataka kuweka sahihi yako nenda katika menu alafu nenda katika Insert > Drawing na kasha chagua “New.”

Hapo ukurasa wa Google Drawing utatokea na uwanja wa wewe kuanza kuweka sahihi yako katika sehumu ya mistari chagua ‘scribble’ (fuata picha hapo chini)

Chora sahihi (signature) yako, hapa unaweza ukachora kwa kutumia mstari mmoja tuu au ukatumia kwa zaidi ya mmoja.
Hapa ukitaka kufurahia Zaidi uwe na kifaa ambacho kinatumia peni spesheli kama vile matoleo mengi ya Samsung Note (mengi ya peni hiyo) au hata baadhi ya iPad zina peni spesheli.
Baada ya hapo uneweza mwenyewe kuanza kubadilisha rangi za mistari hiyo, ukubwa na kadhalika kulingana na wewe mwenyewe unavyotaka.

Ukipenda sahihi hiyo na kama unaona iko tayari unaweza ukaihifadhi kwa kuchagua ‘Save and Close’
Ukurasa huo utajifunga na sahihi hiyo itakuja moja kwa moja katika eneo la uwanjani katika google doc husika

Hapo unaweza sogeza sahihi hiyo katika eneo ambalo unataka ikae… mfano unaweza ukawa umeandika barua na kuisogeza pale kwa chini.
Mpaka hapo utakua umeshafanikisha jambo hili, furahia maujanja hayo sasa
Nindikie hapo chini katika uwanja wa comment, hii umeishawahi kuitumia au ndio leo tunakujuza? Ningependa kusikia kutoka kwako.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.