Korea Ya Kaskazini ni nchi yenye msimamo mkali na pengine wa kipekee zaidi duniani. Nchi hii inayoendeshwa kijeshi imetengeneza mfumo-endeshaji wao wa kompyuta ambao unashabihina na mfumo wao wa kisiasa – wa usiri, wa kipekee na iliokuwa na shuruti, kutokana na maneno ya watafiti wawili wa kijerumani ambao wameuangalia mfumo huo kiundani.
Red Star
Mfumo-endeshaji wa Korea ya Kaskazini umepewa jina la Red Star na umetengenezwa kwa ufadhili wa serikali. Taarifa ya watafiti, Niklaus Scheiss na Florian Grunow wa kampuni ya kiusalama ya Kijerumani ya ERNW GmbH ilitolewa kwenye Chaos Communication Congress, ambao ni mkutano wa wadukuzi na watafiti wa usalama.
Kiongozi mkuu wa nchi hii ya Korea aliyefariki, Kim Jong-iI aliwahi kusema kwamba North Korea inafaa kutengeneza mfumo wao wenyewe wa kompyuta, na hichi ndicho walichofanya sasa. Mfumo wao haujiungi na mtandao mwingine wowote nje ya North Korea lakini unaruhusu kujiunga na tovuti zilizoruhusiwa na serikali pamoja na zile za serikali. Mfumo huo umekuwa ukitengenezwa kwa miaka kumi sasa.
Mfumo huo umetengenezwa kwa kutumia “code” za Linux Fedora na umeonekana kuwa na muonekano wa mfumo wa kompyuta za Apple Macs. Inaonekana mfumo huo umetengenezwa kuzuia namna yoyote ya kuingiliwa na wadukuzi wa nje ya Korea ya Kaskazini. Watu wengi waliowahi kuingia Korea wanasema ya kwamba Windows XP ndio inayotumika zaidi.
Cha muhimu zaidi, mfumo huu umetengenezwa kuzuia usambazaji wa movie za mataifa mengine na miziki kwa kutumia USB kwani Red Star inaweka alama kwa kila faili kwenye kompyuta na linalotumwa kwenda kwenye kompyuta nyingine, kufanya iwe rahisi kumkamata mtu anayesambaza mafaili yanayokatazwa na serikali.
Watafiti hao wanasema ya kwamba hii ni kutokana na serikali kutambua kwamba inahitaji njia mpya za kuwabana wananchi wake dhidi ya kupata mawazoo kutoka nchi za mbali, ikiwemo nchi za magharibi.
Kama unajiuliza kwamba huu mfumo umejengwa na uwezo gani basi, jibu ni kwamba mfumo huu umejengwa kwa ajili ya kumruhusu mtu kufanya mambo machache muhimu, kama kuandika nyaraka, kuangalia kalenda na kutayarisha muziki.
Korea ya Kaskazini si nchi pekee yenye mfumo wao wenyewe wa kompyuta. Kwa mujibu wa makala ya Reuters, Cuba wana mfumo uitwayo National Nova, wakati China, Urusi na wengine wamejaribu kutengeneza za kwao.
Chanzo: Reuters
No Comment! Be the first one.