Google Finance ni tovuti maalum ya Google kwaajili ya habari za kibiashara pamoja na taarifa za kifedha. Tovuti hii ilianzishwa na Google mwaka 2006 na inasaidia watumiaji kuona dhamani za hela, Utendaji wa sekta mbalimbali katika soko la Marekani, Orodha ya masoko bora na habari muhimu za kibiashara.
Kama wewe ni mwekezaji au unataka kuanza uwekezaji basi Google Finance ni tovuti nzuri kwako na itakufaa katika ufuatiliaji wa dhamani za hisa za makampuni mbalimbali duniani pamoja na taarifa mbalimbali zinazoweza kuadhiri soko la hisa hizo. Ifahamike kuwa tovuti hii haina sehemu ya kukuwezesha wewe kununua hisa bali ina taarifa na maelezo yatakayokuongoza katika kuchagua kampuni ipi ya kununua hisa zao. Muundo wa Google Finance upo kama ifuatavyo.
Sehemu ya Kulinganisha Masoko: Katika tovuti ya Google Finance sehemu ya juu kabisa ni sehemu ya kulinganishia masoko ambapo mtumiaji ataweza kulinganisha masoko ya hisa kulingana na muda mfano (siku, wiki, mwezi na mwaka), Bara (Ulaya na Asia) pamoja na aina ya soko (Soko la hisa, Dhamani ya hela pamoja na Dhamani ya sarafu za kidigitali).
Sehemu ya Kutafuta: Sehemu hii humsaidia mtumiaji kutafuta na kupata taarifa zozote za kifedha kama taarifa za soko la hisa la kampuni au kiwango halisi cha ubadilishaji wa hela.
Kalenda ya mapato: Ni ratiba ya robo mwaka inayoonyesha tarehe za kutolewa kwa ripoti za fedha zilizo na taarifa ya utendaji wa mashirika yanayouza hisa. Kupitia Google Finance utaweza kuona tarehe halisi za ripoti hizi za mashirika kuachiwa na utaweza kufanya ufuatiliaji wa kina zaidi kupitia maelezo yaliyopo kwenye ripoti hizo.
Habari za kifedha: Hizi ni habari mbalimbali ambazo zinaweza kuadhiri soko la hisa za kampuni flani. Kupitia tovuti hii ya Google utaweza kupata habari mbalimbali zinazoadhiri soko la hisa ulizochagua kufuatilia na kukuwezesha mtumiaji kuwahi kufanya maamuzi yatakayolinda uwekezaji wako. Habari zinazopatikana hapa hutokea katika tovuti mbalimbali ikiwemo CNBC na tovuti zingine nyingi za kibiashara.
Mwenendo wa soko: Kupitia tovuti hii utaweza kuona mwenendo halisi wa masoko ya hisa kwa muda halisi. Utaweza kupata taarifa kama hisa zipi zinapanda sana sokoni, zipi zinashuka sana sokoni na taarifa zingine nyingi za kuhusu masoko ya hisa.
No Comment! Be the first one.