Watu wengi wanadhani kuwa michezo ya kompyuta imeandaliwa kwa ajili ya baadhi ya wachezaji tu, wanaojua na kulewa kucheza michezo hiyo; na ni rahisi kuelewa ni kwa nini. Michezo mingi inayoandaliwa ni maarufu na kwa ajili ya makundi fulani ya watu.
Hii ni michezo mitano maarufu ya Windows 10, ambayo ni rahisi na mara zote mitamu kuicheza.
Mfano, wiki hii, EA SPORTS wameachia FIFA 16, mchezo maarufu wa mpira unaochezwa na mamilioni ya watu duniani kote. Au mchezo wa magari ya NEED FOR SPEED, GTA V, au mchezo maarufu wa WORLD OF WARCRAFT. Lakini, si watu wote wanapenda michezo ya aina hii. Michezo inayoumiza ubongo na kutumia muda mwingi kuicheza. Kuna watu wanapenda michezo rahisi, isiyohitaji akili na muda mwingi kuicheza. Hii ni michezo mitano maarufu ya Windows 10, ambayo ni rahisi na mara zote mitamu kuicheza.
Lara Croft GO
Kila mmoja wetu anapenda kucheza mchezo wa Tomb Rider. Ni raha, unavutia na mchezaji wake ni noma sana. Waandaaji wa mchezo huu, Square Enix wanajua kitu watu wanapenda, na safari hii wameongeza misheni mpya na za kuvutia kumpeleka mchezaji Lara Croft kukamilishwa misheni hizo. Utatakiwa kutafuta njia mpya za kufikia ustaarabu wa kibinadamu, kufumbua mafumbo kupata njia mpya n.k. Kupitia Windows 10, sasa unaweza kucheza kupitia Kompyuta au simu yako ya mkononi yenye windows hii.
March of Empires
Mchezo mwingine ambao ulitengenezwa kuweza kuchezwa sawa kwenye simu kama unavyochezwa kwenye kompyuta, March of Empires. Moja ya mchezo maarufu zaidi kutoka Game Loft. Katika mchezo huu, utachagua, labda unataka kuwa Mfalme wa Milimani, Sultani wa jangwani au Kiongozi wa kaskazini kisha, kuchagua wafanyakazi wako wakusaidie kuipa nguvu na mipaka ngome yako. Lengo kuu la mchezo ni kushinda vita junavyovianziasha kwa ajili ya ngome yako, na mchezo huu ni mzuri sana kwa watu wanaopenda micezo ya kutumia akili.
Mahjong Secrets HD
Huu ni mchezo mzuri sana kwa watu wanaopenda kucheza magemu lakini hawataki kuwa na mwendelezo wa michezo hiyo. Mahjong Secret HD inakujia na michezo zaidi ya 100 amayo inatofautiana kwa kila hatua ya mchezo. Hata kwa watu ambao hawajawahi kucheza kabisa Mahjong wanaweza kufurahia kujifunza sharia na ujuzi wa kushinda kila hatua ya mchezo. Kitu kingine kinachovutia na kuupa mchezo huu utamu, ni kwamba Mahjong una vitu mbalimbali vilivyofichwa pamoja na michezo ya bonsai itakayokupa alama nzuri kusonga mbele.
Dumb Ways to Die 2: The Games
Huu huenda ukawa mchezo mkali kuliko yote. Mchezo mkubwa zaidi unaweza kuwa na kama michezo midogo 30 ambayo ni lazima uimalize ili kushinda mchezo. Unachezaje? Mchezaji wako ambaye ni tufe, hana akili kuliko wengine wote katika kijiji. Utacheza kuishi lakini utapata matatizo au kufa kwa vitu kama kuzuiwa njia, miiba au vikwazo vingine vya mchezo na utaonekana shujaa wakati wa kupita vikwazo vingine vya hatari kama vile fnsi za umeme n.k. mcehzo hhuu unahitaji akili sana, lakini ni mzuri, mrahisi na unachangamsha akili. Unafaa kuchezwa ofisini wakati mtu amechoka.
9 Clues 2: The Ward
Unapenda michezo ya hadithi ambayo inakuweka katika upande mzuri wakati wa mchezo. Mchezo ambao utakua kuna wakati unaogopa kidogo? Mchezo ambao hauna mambo ya kulipishwa ili kuweza kufungua hatua nyingine ya mchezo? Kama unapenda hivyo vyote, basi 9 Clues 2 unakufaa kabisa. Katika mchezo huu, unachofanya ni kutafuta hasa nini kinaendelea katika makazi ya Mnemosyne yaloyowahi kuteketezwa na moto miaka mine iliyopita. Vitu vichache vilivyosalia ndivyo unatakiwa ucheze nae kujua chanzo, nini kilitokea na wahusika. Unaweza kucheza?
Kupata michezo hii, nenda katika Store yako ya Windows 10, na andika jina mojawapo la michezo hii katika sehemu ya kutafuta na shusha mchezo ili kuucheza.
Chanzo cha Makala haya ni WindowsCentral.com
No Comment! Be the first one.