Kwa wengi bila ya shaka washasikia neno linalotamkwa kwa herufi tatu la APK. Kama hujawahi kulisikia lakini pengine umeliona sehemu kadhaa limeandikwa. Aidha kwenye simu yako au kupitia mitandao ya kijamii.
Pamoja na yote hayo mawili huenda ukawa hujafahamu lolote kuhusiana na APK. Kwa wale ambao hawana ufahamu wowote basi kupitia hapa Teknokona tutakufahamisha kwa njia fupi na yenye kueleweka.
APK ni kifupisho cha ‘Android Application Package’. Yaani ni mfumo maalumu wa teknolojia hifadhi wa apps kwa zinazotumika katika simu zinazotumia mfumo endeshi wa Android.

Programu za APK zinatumika kwenye simu za Android tu na si vinginevyo. Ingawa unaweza tumia kwenye kompyuta kama utaweka programu spesheli za utumiaji wa apps za Android kwenye kompyuta. Pia kompyuta za kisasa za Chrome OS kutoka Google zinauwezo pia wa kutumia app za Android.. Unapozungumzia programu za APK ni kama unazungumzia programu za Windows ambazo faili zake huwa mwisho zinakuwa na anuani ya .EXE.
Unavyodownload app kama za WhatsApp, Facebook n.k. kwenye simu yako ya Android faili linalodownloadiwa linakuwa kwenye mfumo wa APK.
Na programu za APK hupatikana zaidi na ndio rasmi kwenye Google Play Store. Lakini yapo masoko mengine rasmi na yasiyo rasmi yanakupa uwezo wa kudownload app za mfumo wa APK, mfano ipo mitandao kama apkmirror.com, apkpure.com, f-droid.org na nyinginezo nyingi unazoweza kupata programu za APK.
Lakini inashauriwa sana kutumia APK zinazopatikana ndani ya Google Play store kwa ajili ya usalama wa simu yako kuepukana na virusi wanaoweza kuwekwa kupitia programu ambazo zinapatikana nje ya Play Store.
Namna ya kuweka programu za APK kwenye simu yako ni rahisi sana. Ni zoezi linalofanywa na wengi takribani kila siku. Ni vile unavyoingia Play Store na kutafuta progrmu unayoitaka na kisha kuanza kuipakua (Download) na baadae yenyewe inaanza kuinstall autoamtic.
Aidha kwa programu zilizo nje ya Paly Store itabidi kwenye simu yako uingie kwenye Settings, eneo la security na uruhusu unknown Sources ili uweze kuinstall programu za APK. Fahamu zaidi hapa – Teknokona -> Downl0ad app nje ya Google PlayStore