Adobe ni kampuni ya kimataifa inayohusika na utengenezaji wa programu mbalimbali za kompyuta maalum kwaajili ya kuunda michoro (Graphics), picha, video, sauti na programu za uchapishaji. Programu za kompyuta zinazotengenezwa na Adobe zimegawanyika katika makundi yafuatayo, Programu za kuunda michoro, proramu za kutengeneza tovuti, programu za kuunda video na makundi mengine mengi.
Miongoni mwa makundi hayo ya programu za Adobe programu za kuunda michoro ndo zipo nyingi zaidi. Orodha ya programu zote za Adobe ni kama ifuatavyo.
Adobe Photoshop: Hii ni programu ya kompyuta maalum kwaajili ya kuhariri picha mbalimbali kwa kuzibadilisha muonekano au kuongezea baadhi ya vitu. Kwa kutumia programu hii utaweza kuhariri picha kwa kuziongezea mwanga, kuondoa vitu mbalimbali kwenye picha na mambo mengine mengi.
Adobe Illustrator: Hii ni programu ya kitaalamu inayotumika katika ubunifu na uchoraji. Adobe Illustrator inatumika kama sehemu ya mtiririko mkubwa wa kazi, Illustrator inaruhusu kuunda kila kitu kutoka kwenye vipengele vya muundo mmoja hadi utunzi mzima. Wabunifu hutumia Illustrator kuunda mabango, alama, nembo na mambo mengine mengi.
Adobe Premiere Pro: Ni programu ya kompyuta maalumu kwaajili ya kuhariri video katika ubora wa hali ya juu. Programu hii pia inatoa uwezo wa kuhariri sauti za mazingira ya video inayohaririwa pamoja na upachikaji wa miundo mbalimbali ndani ya video.
Adobe After Effect: Hii ni programu ya kwenye kompyuta inayohusika na uchanganyaji wa safu nyingi za video na picha kwenye eneo moja. Programu hii pia inampa mbunifu uwezo wa kupachika miundo mbalimbali ndani ya Video pamoja na picha.
Adobe Audition: Ni programu ya kompyuta maalum kwaajili ya kurekodi, kuchanganya na pia kuhariri sauti. Kwa kutumia programu hii utaweza kuunda sauti mbalimbali au kuunganisha vipande vya sauti pamoja na mambo mengine mengi.
Zipo programu zingine nyingi za Adobe ambazo hazijaelezewa katika makala hii ikiwemo Adobe Lightroom, Adobe Dreamweaver, Adobe Acrobat nk.
No Comment! Be the first one.