Je muda umefika umeona mtandao wa Facebook haukufai tena? au unataka kuchukua likizo tuu, kujiondoa bila kufuta akaunti yako moja kwa moja?
Mtandao wa Facebook unawapatia watumiaje wake uwezo wa kufuta kabisa akaunti zao na pia uwezo wa kuzima akaunti tuu na kutopatikana kwa kipindi flani hadi pale mwenyewe utakapotaka kurudi hewani.
1. Kuzima akaunti yako (Deactiving) – yaani kuondoa akaunti yako mtandaoni na kutopatikana kwa watu wengine.
2. Kufuta akaunti yako moja kwa moja (Deleting).
Vyote viwili vinatofauti zake, hasara na faida yake kulingana na malengo yako hasa.
Futa kabisa (Delete)
Kama una nia ya kuondoka na kutorudi kamwe katika mtandao huo basi unaweza futa.
Utapewa chaguo la kuweza kushusha (download) mafaili yako yote, kama vile picha, kabla ya akaunti hiyo kufutwa moja kwa moja.
Muhimu kujua;
- Ujumbe (meseji) ulizochati na watu, kwako zitafutika lakini kwenye upande wa wapokeaji wa meseji hizo bado watabakia na mazungumzo yenu. Ila hawataweza kujibu tena.
- Picha, status, ujumbe (comment) uliochangia kwenye makundi na kurasa (page) vyote vitafutika.
- Utaratibu mzima wa kufuta akaunti yako utaanza mara moja baada ya wewe kuomba hilo litokee ila tukio zima litachukua hadi siku 90 kwa kuwa data zako zinahifadhiwa katika kompyuta kadhaa za uhifadhi data za mtandao huo. Ila katika hizo siku 90 tayari watu hawataweza kuona akaunti yako wala vitu vyako kama vile picha n.k.
- Akaunti ikishafutwa ndio basi tena, kurudi tena kwenye mtandao huo itakubidi kufungua akaunti upya na kuanza upya.

Zima Akaunti (Deactivating)
Kama tulivyogusia hapo juu, hili ni kufanya akaunti yako ya Facebook isipatekane kabisa mtandaoni ingawa wewe mwenyewe bado utaweza kuingia (log in) na kurudisha akaunti yako.
Muhimu Kujua;
- Ukichagua ‘deactivating’ Facebook wanachofanya ni kuondoa akaunti yako katika akaunti zinazopatikana kwa watumiaji wake mtandaoni humo
- Hii ina maana watu hawataweza kukutafuta na kukupata kwenye mtandao huo, hawataweza kuangalia ‘Timeline’ (profile) yako.
- Siku yeyote ukijisikia kurudi basi akaunti yako itarudishwa kama ilivyokuwa zamani bila kupoteza data zako zozote.
- Hii ni nzuri kwa mtu anayejisikia anaitaji muda kuwa nje ya mtandao huo.
Bofya Kusoma Makala Yetu ya – JINSI YA KUZIMA (DEACTIVATE) AU KUFUTA AKAUNTI YA FACEBOOK
Je umejifunza kitu leo? Ushawahi kufikiria kujitoa kutoka kwenye mtandao huo? Endelea kutembelea mtandao wetu, kumbuka kuungana nasi pia kupitia Twitter, Instagram na Facebook (kama bado upo 🙂 )
One Comment