Nintendo ni moja kati ya makampuni makubwa kabisa katika maswala mazima ya magemu, kampuni ina magemu mengi ambayo inayamiliki ikiwemo lile maarufu kabisa la Super Mario.
Kupitia Super Mario, kampuni ya Nintendo imejikuta ikipata faida ya 52% zaidi ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Ongezeko la faida hilo limetokea baada ya filamu ya Super Mario kutolewa na kufanya vizuri katika soko hali ambayo ilipelekea uhitaji wa vifaa vya Nintendo Switch kuongezeka kwa kasi.
Vifaa hivyo vya Switch, ni vifaa vya Nintendo ambavyo vinatumika kuchezea magumu kadha wa kadha ikiwemo na yale ya Nintendo.
Wataalam wa mambo pia wanasema ongezeko hilo halijatokana na filamu ya Super Mario tuu bali hata gemu jipya linalojulikana kama Zelda limechangia katika ongezeko hilo.
Ni wazi kwamba filamu hiyo imefanya vizuri sana katika soko na mpaka sasa ikiwa imeingiza zaidi ya dola bilioni 1.3 za kimarekani kama sehemu ya mauzo.
Mbali na hapo bado hii inakua ni moja kati ya filamu zenye mauzo makubwa sana na haswa ukizingatia ni kwamba imetokana na gemu mpaka kwenda katika filamu.
Kingine ni kwamba kampuni ya Nintendo inasema bado inaendelea kujipanga katika kuhakikisha kwamba wanakuza mauzo yao kwa kiasi kikubwa sana.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hili umeipokeaje? Unadhani kampuni itazidi kupata faida kubwa zaidi ya hapa?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.