Uchunguzi unaonyesha kuwa takribani watu milioni 90 ambao wanatumia App za mahusiano (Dating Apps) ambazo zinaonyesha maeneo (Locations) zao, kama vile Tinder na Momo mwezi uliopita. Na ikagundulika kuwa karibia robo tatu ya watumiaji ni wanaume.Kampuni ya utafiti ya GlobalWebIndex imefanya utafiti katika nchi 32 na imepata taarifa kuwa 62% ya watumiaji wa App za mahusiano ni wanaume.
Habari hii sio ya kushangaza sana. Mwaka 2013, kituo cha uchunguzi ‘Pew Research Center‘ kiligundua kuwa wanaume ndio wako ‘active’ katika App na tovuti za Mahusiano. 13% ya wanaume wa Amerika wanatumia App na tovuti za mahusiano wakati 9% tuu ya wanawake ndio wanajihusisha na mambo hayo.
Japokuwa hiyo haimaanishi wanume ndio wanatumia muda mwingi ndani ya App na tovuti hizo kulinganisha na wanawake. Mtandao wa Tinder ambao ‘New York Times‘ imeufanyia makasio/makadirio kuwa una zaidi ya watumiaji milioni 50 walioko ‘Active’. Wakati wanaume wanatumia wastani dakika 7.2 katika matumizi ya App, Wanawake wanatumia Wastani wa dakika 8.5 katika kutumia App hiyo.
No Comment! Be the first one.